Sehemu ya Ziwa Victoria ikioneakana mapema leo kutoka eneo la Soko la Samaki Kirumba Mwaloni,ndani ya Manispaa ya Ilemela.
 Ngalawa ikiwa imesheheni mizigo ikitokea visiwani ikielekea kutia nanga kwenye bandari ndogo ya eneo la Soko la Samaki Kirumba Mwaloni,ndani ya Manispaa ya Ilemela.Globu ya Jamii ilizungumza na watu kadhaa waliokuwepo eneo hilo kuhusiana na usafiri wa Ngalawa kwa ziwa Victoria,walibainisha kuwa usafiri wa Ngalawa ni msaada mkubwa wa usafiri wa mizigo na abiria ndani ya ziwa victoria kwa asilimia kubwa,na wengi wamekuwa wakiutegemea zaidi katika suala zima la kusafirisha mizigo yao kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Ngalawa ya Magunila ikitia nanga tayari kwa kushusha mizigo.
Mizigo mbalimbali ikishushwa kutoka kwenye Ngalawa hiyo,ikiwemo magunia ya dagaa ambayo yalikywa yamefunikwa kama uonavyo pichani,ukiachilia mizigo mingine iliyokuwa ikishushwa kama ionekanvyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2013

    Ankal hivi hawa maripota zako wanatoka Rwanda au wapi?
    Hizi sio Ngarawa(Ngalawa) hizi ni mashua au madau.Kama muandishi wa habari hajui kiswahili sahihi itakuwaje kukienzi Kiswahili?
    Hii ni aibu Ankal unatutia aibu bwana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2013

    Du haya mapipa ni matupu au yana kitu ndani??iwapo kama yana kitu basi ni hatari sana kwa jinsi yalivyopakiwa.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa mwanzo kabisa huko juu, nadhani tuangalie tofauti kati ya BOTI zinazotumia mashine kuendeshwa, NGALAWA au NgaRawa kama waziitavyo wenzetu wa visiwani, hizo huenda kwa kupigwa Makasia, na MASHUWA/MASHUA siku zote hubainika kwa muonekano wa 'Tanga' ambalo husaidia katika mwendo wake. Sasa wewe unapokosowa na kusema hiyo ni Mashua, mie binafsi naona pia umeagulia sivyo, hizo pichani ni boti japokuwa na Mashuwa pia zipo katika Ziwa hilo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2013

    Ankal, hii sio Ngalawa. Naomba kuchangia.Ngalawa huwa na mabao pembeni yaliundwa vizuri mfano wa mabawa pembeni ya chombo hicho ili kukipa balance ya kuelea vizuri kikiwa baharini. sifa ya ngalawa huwa haizami kirahisi na kabisakabisa hata ikijaa maji ndani.kawaulize wavuvi wa mwambao wa pwani utaelewa zaidi.

    Ngalawa hutumia tanga yaani kitamba kikubwa kinachotegemea upepo kwa kukiendesha chombo kikiwa baharini. inawezekana kutumia mshine,lakini tanga ndio asili yake. zaidi manahodha wa chombo hiki wanaelewa.

    Chombo hiki kwa uzoefu wa mwambo wa pwani huundwa kwa jiti kubwa kwa kuchimbwa au kuchongwa kwa shoka hadi kupata umbile likusudiwalo na huwa ni jembamba na sio kama hii yako hapa pichani. Muembe ndio maarufu zaidi kuchongea ngalawa.

    Ngalawa haiundwi kwa kupangiliza mabao na misumari bali hukalafatiwa na kupakwa sifa ili kuzuwiya kuoza na kupenyeza maji ndani. Misumari hutumika tu pale inapobidi tena ni kwa sehemu chache sana.Sifa ni dawa maalumu.

    Asili ya ngalwa ni kwa wavuvi wanaotumia madema na mishipi kwa kutengea samaki na sio kusafirisha mizigo hata hivyo inaweza kupakia mizigo kwa kiasi chake.

    Nadhani nimetowa mchango wangu kwa kiasi ili kuielewa Ngalawa. Ombi langu kwako ni kukipa nafasi kiswahili ndani ya blong yako ya kimataifa ili kukuza na kukieneza zaidi kiswahili asili.

    ushauri: Ukurasa maalumu unahitajika katika blong ya jamii ili wasomaji wachangie katika kukiezi na kukijenga kiswahili lugha yetu kama ilivyo kwa kurasa nyengine..

    Ahsante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...