Mwishoni mwa wiki NMB ilifadhili mkutano wa makampuni na taasisi ambazo wamepewa dhamana ya uchimbaji na usambazaji wa mafuta na gesi nchini. Mkutano huo ulifanyika katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam kwa siku mbili ukiambatana na maonyesho ya biashara kutoka makampuni tofauti nchini Tanzania.

Dhumuni kubwa la mkutano huu lilikuwa ni kutengeneza mahusiano baina ya wafanya biashara na kujadili jinsi ambavyo huduma zitolewazo na makampuni na taasisi zilizopewa dhamana ya uchimbaji na usambazaji wa mafuta na gesi nchini zinavyoweza kuisaidia jamii husika.

 Mkuu wa kitengo cha huduma za miamala kwa taasisi NMB, Gerald Kamugisha akielezea jinsi NMB inavyoweza kusaidia makampuni na taasisi mbali mbali zinazosambaza mafuta na gesi nchini Tanzania.

Kamishina wa Nishati na masuala ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hosea Mbise, akimkabidhi cheti Mkuu wa kitengo cha huduma za miamala kwa taasisi NMB, Gerald kamugisha kwa udhamini ambao NMB umetoa ili kufanikisha mkutano huo.

Meneja ukuzaji wa biashara NMB, Masato Wasira akiwaelezea baadhi ya washiriki wa mkutano huo juu ya huduma zitolewazo na benki ya NMB

Sehemu ya washiriki wa mkutano wakisikiliza kwa makini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...