https://encrypted-tbn0.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcScmZm1uZbbqL1n5aRJc62mHsWwFM8e-dO2eoNTl43Cx-PCaCMJ9Q  
Rais Paul Kagame wa Rwanda.

ONYO lililotolewa na Ikulu ya Marekani dhidi ya Serikali ya Rwanda, linalomtaka Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame, kuacha kuwasaidia waasi wa kikundi cha M23, lina kila dalili zinazomuweka kwenye kundi la viongozi wa Kiafrika ambao hatma yao baada ya kuachia madaraka inazungukwa na wingu la mashaka.
Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye mapema wiki hii alikaririwa na vyombo vya habari mbalimbali duniani akimtaka Rais Kagame kuacha kukisaidia kijeshi kikundi cha waasi wa M23, anaaminika kuitoa kauli hiyo kama msimamo wa serikali yake inayopinga watawala wanaojihusisha na uhalifu wa kivita.
Ingawa hadi sasa Rais Kagame hajatajwa na Ikulu ya Marekani kama mmoja wa viongozi wa Afrika wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita, onyo lililotolewa na Rais Obama linadhihirisha kuwepo kwa ushahidi unaomhusisha na matukio ya aina hiyo yaliyopata kuwagharimu baadhi ya marais walionyooshewa kidole na Marekani kwa aina hii hii anayonyooshewa sasa Kagame.

Wadadisi na wafuatiliaji wa mambo walioichambua kauli ya Rais Obama, wanaeleza kuwa aliitoa baada ya Marekani kujiridhisha na ushahidi ilioukusanya ukiihusisha Serikali ya Rwanda kuwasaidia waasi wa kundi la M23.
Wanaeleza kuwa Marekani baada ya kubaini ushirika wa majeshi ya Rwanda yaliyojipenyeza ndani ya makundi ya waasi wanaopigana na Serikali ya Kongo, huku wakitekeleza vitendo vya kinyama dhidi ya binadamu katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini, imeamua kumtosa Kagame, ambaye amekuwa na uswahiba wa muda mrefu na taifa hilo.
Katika tathimini yao kuhusu uzito wa onyo la Rais Obama kwa Rais Kagame, wanaeleza kuwa hataweza kuepuka kitanzi cha mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Waasi wa kikundi cha M23, mbali na kuendesha mapambano dhidi ya majeshi ya Serikali ya Kongo, jambo linalopingwa na jumuiya ya kimataifa, pia wanatuhumiwa kwa ubakaji na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Tuhuma hizo pia zinaelekezwa kwa majeshi ya Rwanda, yanayodaiwa kushirikiana na waasi hao na ndizo zinazomuweka Rais Kagame katika hatari ya kufikishwa mahakamani na hata kuhukumiwa kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Rais wa Liberia, Charles Taylor.
Taylor  kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 50 jela baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone ambako zaidi ya watu 50,000 waliuawa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe na wengine wengi wakiachwa na ulemavu wa kudumu.
Kama inavyotokea kwa Rais Kagame sasa, kwa Taylor pia ilikuwa hivyo hivyo, pale alipokuwa akionywa na jumuiya za kimataifa na yeye kudharau maonyo hayo.
Wakati wadadisi na wachambuzi wa mambo wakiwa na mtizamo huo kuhusu onyo la Serikali ya Marekani dhidi ya Rais Kagame kujiingiza kijeshi katika vita vya ndani ya Kongo, ushahidi uliokusanywa na taasisi za Umoja ya Mataifa za kutoa misaada ya kibinadamu unaonyesha kuwa wanajeshi wa Rwanda wanaopigana bega kwa bega na waasi wa M23 wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kihalifu dhidi ya binadamu.
Ni ushahidi wa aina hiyo ndio uliotumiwa na ICC, kumhukumu Taylor, aliyekuwa akituhumiwa kuvisaidia vikundi vya waasi vya Revolutionary United Front (RUF) na Armed Forces Revolutionary Council (AFRC) kwa kuvigawia silaha za kivita kwa muktadha wa kupewa madini ya almasi.


CHANZO:  Mtanzania Jumapili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2013

    Rais Kagame amecheleweshwa sana kwenda ICC akilinganishwa na marais wengine kama wa Sudan ambaye ushahidi ni mdogo. Kagame amehusishwa toka kifo cha Habyalimana pia vita ya Kongo na ushahidi ni mkubwa sana! Si mnajua Nkunda alijisalimisha kwa Kagame na akamficha, tunahitaji ushahidi gani zaidi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2013

    HAKUNA HAJA YA KUSUBIRI MAREKANI, SISI´WENYEWE TWENDE MPAKA HUKO KWAKE TUPIGE TUMTOE KAMA NDULI IDDI AMIN, FALA MMOJA KAMA HUYO KWANZA ANAUMWA KWASHAKOO RAIS GANI ASIENENEPA KWA SABABU YA ROHO MBAYA.

    SWAIN KWANZA WANYARWANDA WOTE FUKUZILIA MBALI HAPA KWETU BONGO

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2013

    Kama Kagame mbabe afanye kwa Rais wa dunia au anabweka kwa Rais wetu Kikwete tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 30, 2013

    Paul Kagame wa Rwanda hana tofauti ba Charles Tylor liyekuwa Liberia.

    Kama Taylor alotoa silaha kwa Makundi ya Waasi wa Sierra Leone RUF na AFRC ili apewe Alamsi, vivyo hivyo Paul Kagame anapiganisha Waasi wa M23 ili avune Madini Mashariki ya Kongo-DRC.

    Na ndivyo alivyofanya Jonas Savimbi kule Angola akitoa silaha Waasi waendeshe vita ili yeye Savimbi avune Almasi za Angola na kujitajirisha.

    Inavyoonyesha Savimbi hakuwa na mahitaji sana ya Utawala na Madaraka balilengo lake lilikuwa ni Utajiri kwa biashara ya Almasi za damu!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 30, 2013

    Kagame uacheza na Obama wewe?

    Unavyojifanya unaijua sana vita ya Msituni utatandikwa na Drones 'Madege yasiyo na Marubani' ya Marekani.

    Fanya mchezo uone utastukia Madege yapo juu ya anga Kigali ushindwe pa kukimbilia!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 30, 2013

    Kagame ukifanya mchezo hiyo nchi yako Obama atamkabidhi Jakaya Kikwete aongoze idadi ya Mikoa ya Tanzania!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 30, 2013

    Kweli nyani haoni kundule, ni huyu huyu Obama ambaye amesupport waasi wa Libya kumuondoa Rais Gaddafi ambaye alikuwa ameleta maendeleo makubwa nchini mwake na bila ya mikopo na misaada ya magharibi sasa ana support waasi wa Syria kumuondoa Rais Assad ambae ana zaidi ya 75% support ya wananchi wake sasa hivi anamtishia Kagame? Labda kwa sababu analeta maendeleo makubwa nchini mwake bila ya mikopo ya IMF na World Bank, inabidi uwe na upeo kuona nia na madhumuni ya nchi za magharibi kumbukeni ni wao peke yao ambao kwa zaidi ya miaka 10 sasa hawana maendeleo ya kiuchumi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 30, 2013

    Eti anadai kama yeye Mtusi alivyoweza kuwatawala Wahutu waliowengi nchini kwake anaweza kumtawala kila mtu mwingine!!! Ama kweli ana kazi!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 30, 2013

    tatizo baba wa taifa mwalimu JNK
    amewalea saana hawa wa-rwanda sasa
    wamejisahau kama tanzania ya sasa ipo tofauti na ya miaka ya malezi
    waliopewa na baba wa taifa. Nakubaliana na mdau wa hapo juu
    hakuna haja ya kumngojea Obama
    amfikishe PK ICC watanzania wenyewe
    tunaiweza kazi ya kuilinda nchi yetu tena hatutoishia mipakani wanajeshi wetu gwaride la "march-over" chai ya asubuhi mjini kigali.
    mikidadi-denmark

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 30, 2013

    Kagame hana pa kukunbilia siku kikiumana kwangu sikutaki kwetu usije kabisa pa kwenda ni ICC tuu.Wewe unacheza na TZ moto wa Kuotea mbali,kumbuka TZ wana uhusiano mzuri na Nchi zote Duniani ila tu Rwanda na Malawi kidogo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 31, 2013

    Kagame alikalia kuti kavu tangu aangushe ndege iliyomuua Habyarimana na Ntaryamira. Alitakiwa asijihusishe tena na masula ya vita vya kiasi, badala yake aliona anaweza kutanua himaya yake hadi eastern congo...he made big mistake. Kama ana washauri wazuri arudi amwangukie Kikwete na awakabidhi viongozi wa waasi wa congo kwa ICC.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 31, 2013

    marekani ingekuwa dili wangepigwa na matalibani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...