Rais Barack Obama wa nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba na watoto zao,wakiwasili chana huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku mbili hapa nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mchana wa leo. Kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.nyuma ya Rais na mgeni wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama.
Rais Barrack Obama akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku mbili.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana na Rais Barrack Obama katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
RaisDkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwaongoza wageni wao Rais Barrack Obama wa Marekani na mkewe Michelle kuangalia ngoma mbalimbali za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa ziara ya siku mbili nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani wakifurahia na kufuata mapigo ya ngoma za utamaduni katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu jijini Dar es Salaam leo mchana wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo wa Marekani na ujumbe wake.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwatambulisha baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali kwa Rais Barrack Obama na mkewe katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Picha na Freddy Maro,Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. hivi ni kweli hata picha wanapiga wenyewe kisha ndio wagaiye magazetini

    ReplyDelete
  2. Asante kwa picha na maelezo but, professional photographer kama wewe umekosa picha nzuri mpaka unatoa kwenye tv?

    ReplyDelete
  3. Asante kwa picha lakini Professional Photographer kama wewe ni aibu kuweka picha kutoka kwenye tv, hazina muonekano mzuri

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2013

    Michuzi mwenyewe unapiga picha TV screen, chezea America.

    I am glad i am not in Tanzania.

    houston.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2013

    Kaka, kumbe na wewe jina lako limechujwa! naona umepost picha ulizopiga kwenye runinga. Pole sana

    ReplyDelete
  6. Stupid tanzanians. Michuzi mwaya hongera kwa kutuletea habari

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2013

    ha ha ha ha ! Nimecheka sana. Mr Michuzi vipii mjomba? mbona umetuwekewa picha zinazo beep bwana? Picha clear ziko waapi mtu wetu?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2013

    Haha proffesional photographer,unatuwekea picha za tbc,chezea wamerekan wewe,no entry!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2013

    kaka pole wenye dunia wame kudelete kwenye list.Ina maana hawatambui hata ww mpiga picha wa JK.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2013

    Watu wengine bwana.. Mtu amewasaidia kuwapa habari, mnaanza majungu yasiokuwa na mbele wala nyuma.. Anyways, pamoja na kuwepo kwenu huko Marekani lakini ngoja niwaelimishe kidogo (by the way, mimi pia nimeishi States miaka mingi sana). Anyways, Rais wa Marekani (POTUS) ni Rais aliye na ulinzi wa hali ya juu sana kuliko rais mwingine yoyote duniani, nje na ndani ya USA (especially, Obama - kumbuka ana asili ya mtu mweusi).. Kwa kifupi, kuna ugumu wa hali ya juu pia kupiga picha kiholela kwa mambo ya kiusalama zaidi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2013

    Kweli Marekani ogopa. Mswati ulimpiga picha za kuonyesha mpaka "kiatu" gani amevaa. Wa Sri Lanka naye hivyo hivyo. Obama - mmmmmm!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2013

    Asante ankal kwa picha ambaye sina runinga hii imekuwa safi sana. ankal tutasema tutalala, tuwekee kadiri unavyozipata, tusio na runinga tufaidi.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2013

    Picha nzuri!! lakini kwa nini Rais JK ametambulisha viongozi wa serikali ya Zanzibar tu??Yuko wapi PM, spika wa Bunge, mawaziri etc

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 01, 2013

    Asante ndugu michuzi kwa picha NA habari mbali mbali za ujio WA rais Obama haijalishi umezitoa kwenye TV au wapi usivunjike moyo endelea kutuhabarisha uwezavyo.

    ReplyDelete
  15. Security ni muhimu kwa rais kama obama cha msingi kaingia tanzania na tunaomba amalize ziara yake kwa amani hongera uncle michuzi

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 02, 2013

    Asante sana Michuzi kwa picha na maelezo. Sisi wengine tungezionea wapi kama siyo jitihada zako.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 02, 2013

    Bandugu sio tatizo la Michuzi, tusimsakame wala kumthihaki au kumjoki. Inawezekana na yeye bado haamini!
    Ni tatizo la yule/wale wanaodhani kuwa wakati wote na kila mahali kuna maadui wanaotafuta kuwadhuru. Tabia hii ni tabia ya watu wasio wema. Kama mgeni hawezi humuamini mwenyeji wake basi hapo kuna tatizo. Kamwe mgeni hawezi kuijua nyumba kuliko mwenye nayo. Asante sana Michuzi kwa kazi nzuri.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 02, 2013

    chezeya marekani wewe picha unapiga kwenye luninga tu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 02, 2013

    picha nzuri haijalishi umetoa wapi ujumbe umetufikia good work ankali

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 02, 2013

    yaani mtu anayejihami hivi ina mana ana adui wengi sana! Sawli la kujiuliza kwa nini mtu unakuwa na adui wengi? makisio 1. labda unazo sana 2. labda ni mwizi 3. labda ni mchawi kwa filisofia ya kiafrika au labda una shida binafsi!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 02, 2013

    yaani kweli nimeamini watz ni watumwa yaani una clush vya kwenu kisa upo america??

    ReplyDelete
  22. Katika kuwakabidhi Nchi, lazima waingie kwa Vishindo. Bush alivyokuwa Rais hakujua Tanzania ni nini wala iko wapi. Ghafla Tanzania imekuwa mali! Tusijidanganye, Tanzania ni Rasilimali yake. Si kiongozi wala watu sisi. Tulie Tu! Deal imekamilika.
    Shusha huu ujio nyumbani kwako na utafakari, ungekuwa wewe ni mtu wa jinsi gani, hata Mgeni kuteka nyumbani kwako Jumla!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 02, 2013

    taarifaaa...!!!
    huo muziki unaopigwa na kikundi cha Tarumbeta, asiri yake ni Usambaani unafahamika kama "MGHUDULO"; achakabisa ikipigwa kiufasaha haswa na wazee toka fwizai lazima uinuke na kucheza...
    ...nna kadudu mwe moyo...!
    Obama mwenyewe hakusita kucheza si mnamuona kwa picha.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 03, 2013

    Tanzania yangu maskini!INAONDOKA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...