Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Rais na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Makamu na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2013

    Kitendo cha Mheshimiwa Rais kuongozana na mkewe Salma katika matukio mengi, ni mfano wa kuigwa na wengi wa viongozi na familia za kitanzania. Inapendeza sana, inatia matumaini na hakika wanastahili pongezi. Mheshimiwa Rais na mama Salma, mbarikiwe sana na Mungu awazidishie mapenzi na mshikamano wa dhati.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...