Rais mpya wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es Salaam, Rotarian
Ambrose Nshala, akihutubia katika hafla ya kumsimika rais mpya wa
klabu hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Rais huyo
amechaguliwa kwa mwaka wa pili kushika uongozi huo. Wengine kutoka
kushoto ni Gavana Mstaafu, Amu Shah, Theodosia Muhulo ambaye ni mke wa
rais huo na Gavana Msaidizi wa Rotary, Irene Kamau.
Rais wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam, Rotarian Ambrose
Nshala(kulia), akimvisha pini rotarian mpya, Mhandisi Dennis katika
hafla hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Rais wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es Salaam, Rotarian Ambrose
Nshala (kulia), akimpa nyaraka rotarian mpya wa klabu hiyo, Paul
Mashauri katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Rotary klabu ya Mzizima, Rotarian Ambrose Nshala (kushoto)
akiwaongoza wanachama wengine wa klabu hiyo kuselebuka katika hafla ya
kmsimika rais na viongozi wengine wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...