Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Profesa Patrick Makungu akifungua semina ya siku moja ya Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara zote zilizoko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwajengea uelewa pamoja na kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi na misimbo ya posta.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Profesa Patrick Makungu akipongezwa na  Mkurugenzi wa Maswala ya Posta Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Bi. Rehema Makubwi mara baada ya akifungua semina ya siku moja ya Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara zote zilizoko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwajengea uelewa pamoja na kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi na misimbo ya posta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2013

    Semina semina ni ulaji wa ujanja ujanja.Kulikuwa kuna haya gani kuongea na wizara kuhusu matumizi na faida za anwani?haya mambo yalitakiwa kufanywa tokea enzi za Mwinyi huko.Leo hii kutafuta business pahali ni kazi mpaka upate through kuambiwa,"bwanae pale ukikata kona hiv,utaona hoteli nzuri sana ya kitali" haya mambo yameshapitwa na wakti na cha ajabu hawa wakubwa wanatembea kila leo nchi za watu wala hawaoni aibu.

    Kuna faidi nyingi sana kama kukiwa na anwani hapa nitasema kwa ufupi.ila la msingi ni security..serikali lazima waweze kuorodhesha mtu anwani yake na identification card ya mwananchi pia.Hiyo itasaidia mambo mengi sana katika uhalifu na pia ulinzi.

    Kingine ni ukuaji wa sekta ya biashara.Tutegeemee uchumi wa tanzania kukua sana kutokana na approach hii.Hii inamaanna biashara na sehemu zitakuwa kwenye data base na itakuwa rahisi kupata bishara,pia italeta ushindani wa kibiashara ndani na nje ya nchi.

    Nashauri pia serikali iajiri wapangaji mji hata kutoka njee maana hawa tulio nao hawaa upeo.Kuna watanzania wengi wako nje ya nchi wanautaaluma ya hizi vitu mana majiji yamesongamana wakati ardhi tunayo kubwa sana na yakutosha.
    pia itasaidia kupunguza bei za nyumba na pango maana kila mtu anatkaa kukkaa karibu na mjini dar es salama.tukiwa na wapangaji miji wazuri basi na anwani pamoja naamini mambo yatakuwa shwari.

    tuache siasa nakuhubiri .Tufanye kazi kwa bidii.jamani tufanye kazi kwa bidii tujenge nchi yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...