Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. 
 Jumla ya watu 38 wanashiriki zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro lijulikanalo kama Kili Challenge 2013 kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa UKIMWI. 
 Kundi hilo ambalo linaongozwa kwa kiasi kikubwa na wafanyakazi wa kampuni ya kuchimba madini ya  Geita wanaendelea na safari yao wakiwemo watoto 2 walioathirika na maambukizi ya VVU/UKIMWI wanaolelewa na Kituo cha Watoto Yatima cha Moyo wa Huruma wenye umri wa miaka 14 na 17. 
 Katika kundi hilo wamo pia raia sita kutoka Afrika kusini, raia mmoja kutoka Ghana, raia mmoja kutoka Australia na watanzania 27.
 Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akiwasili katia maeneo ya geti la kupandia mlima Kilimanjaro la Novatus Makunga
 Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizungumza na wapanda mlima kutoka Geita Gold Mining.(hawako pichani) wakati wa uzinduzi wa changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangia fedha kwa waathirika wa VVU na UKIMWI.
 Wapanda mlima ambao wengi wao ni wafanyakazi wa Geita Gold Mining wakimsikiliza mgeni rasmi katika changamoto hiyo.
 Wapandaji wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizindua changamoto hiyo mahususi kwa ajili ya kuchangia fedha kwa waathirika wa VVU na UKIMWI.
 Bango la wafadhili
Lango la Machame ambalo hutumika pia kwa kampuni ya Geita Gold Mining kuanzia safari ya kupanda mlima kwa lengo la kuchangisha fedha. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2013

    Kupanda mlima kikawaida safari zake nadhani zinaanzia Marangu mtoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...