Na Alex Kassuwi
Kwa wanakijiji wenzangu, miaka 30 iliyopita nisingeliweza kuamini ninayo yaona na kuishi hivi sasa. Kwa kifupi tuliona wakija kijijini kama mapadri, wataalamu wa mashirika toka nje ama walimu.

 Nilijenga imani kila mzungu ni msomi na tajiri. Nilipohamia ughaibuni nimekuta ni tofauti sana, wapo wazungu wengi mbumbumbu na wanabangaiza tu.

Ushauri kwa dada zangu wanaowinda kuolewa na wazungu "kila king'aacho sio dhahabu"

   Kwa matukio ya Swahili TV mtaani kunani tembelea www.swahilitv.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2013

    waache dada zetu wajipatie japo makaratasi,kwani huku bongo amna mambumbumbu na wabangaizaji?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2013

    And your point is? kama mbumbumbu mbona uanawatumikia?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2013

    Hizo si kazi kama kazi nyingine,sasa wewe ulitaka nani afanye hizo kazi wakati ni nchini kwao??ina maana kama ni mzungu asifanye kazi nyingine yeyote??kumbe hata na wewe ni mbumbuuu kweli...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2013

    Katika kila jamii, wabangaizajo wapo hata wabongo wapo wabangaizaji, mada hii haina mshiko lete taarifa za kitaaluma kuelimisha na kuhamasisha kitaaluma kwanza labda tutaweza kujinasua ktk self development kabla kukimbilia kwa mataifa mengine. Na kwa nini umelenga kinadada tu wapo kinakaka wamelost pia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2013

    Alex Kassuwi ASSALAMA LEKKO zako!

    Umeutumbua Mshipa uliokuwa unawasumbua dada zetu saana, wao wanaamini kila aliye Mweupe ana Fedha!

    Dada zetu wengine wamekataa kuolewa na wenzao wa nyumbani wakipapatikia Wazungu, wengi makubwa yaliwakuta likiwemo la kukutanishwa na Wanyama kama mbwa na mambo mengi tu ya fedheha.

    Kazi kwao kama wana vyoona hapo Wazee wa kazi na brooms mikononi wanasafisha magari.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2013

    Fikra zako hazikuwa sahihi. Nadhani dada wanachotafuta sio huo usomi na utajiri pekee, bali ni maisha kwa ujumla. Sio siri, opportunities zilizopo kwa mzungu - kiuchumi, kijamii, elimu, afya nk popote pale, kwa walio wengi zipo juu ya zile za mswahili.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2013

    Mtoa mada anadharau watu wa matabaka tofauti.Upeo wako wa dunia wakati uko kijijini ulikuwa mdogo.Dunia gani ambayo itakuwa na watu ambao hawafanyi kazi za kawaida? Hao wakina dada wanaopenda wazungu ni mapenzi yao na hayakuhusu.Je kunatofauti gani ya kupenda mtu mweusi au mweupe wenye kipato sawa? Mind your own business.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2013

    Hawa sio wazungu wewe,, acha ushamba,,
    Hawa ni Wakudish......... Sio kila mtu mweupe mzungu, hata mchina na mwarabu utaita mzungu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2013

    Acha ushamba,, hawa ni Wakudish,, si Wazungu
    Hata mchina na mwarabu utaita Mzungu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2013

    Mtoa mada nadhani bado ana upeo ulee aliokuwa nao wakati akiishi kijijini.... na kupewa vimsaada vya hapa na pale vya mapadre.... ambao sikulaumu ila kama umeweza kufika ughaibuni ulipaswa kubadili mtazamo na fukara zako.. bila kunyanyapaa akina dada au wazungu.

    Kumbuka haya mawindo ya akina dada ni yale uliyoyaona kulee kwa machangudoa waliokuwa wakifukuzia watu wa nchi nyingi wakijua kuwa wakiwa pale bongo huwa whatever they went to do wanalipwa hela nzuri. Lakini ukiwajumuisha wakinadada woooote weusi nadhani unaonyesha ni jinsi gani upeo wako bado wa kijijini miaka hiyooo.

    Pili kama wadau mbali mbali walivyosema hapo juu, kila kona ya dunia kuna matabaka mbali mbali na kazi mbali mbali, wasomi na wasio na elimu hata kuandika majina yao hawajui. Hivyo fungua ufahamu wako ndugu. Na kuhusu kazi tena wenzetu huku hawajali kutokana na elimu zao duni wala huwezi kukuta wanabagua kazi kwani kila kazi lazima ifanyike ili mradi mkono uende kunywani na uweze lipa bili. Hence kuna wasafisha jiji, vyoo magari, machinjioni mayaya, wazibua vyoo wazoa taka.. wahasibu nk!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 26, 2013

    Mtoa mada mshamba sana wewe,ndiyo maana unatuonyesha gari yako na pushchair ya mtoto?mjomba haya ni maisha ya kawaida sana,uwe ulaya au bongo mambo yote sawaaa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 26, 2013

    tatizo lenu mnafikiri kila alieolewa na mzungu kafuata fedha, mapenzi hayana macho, unaweza ukampenda yeyote. si bora uolewe na mzungu kuliko kubaki bila ndoa, unaishia kuwa nyumba ndogo na kesi kibao toka kwa mke mkubwa. achene hizo, wakibaki hapa bongo mtawaoa wote? tumieni busara katika kutoa hoja zenu

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 26, 2013

    me nadhani mtoa mada alishabwagwa na mmbongo mwenzie alafu kaenda kwa mzungu, ila wanadamu mna maneno sana angeolewa na mswahili lkn anafanya kazi hiyo ulioonyesha haina shida, sijui uko dunia ya ngapi rafiki

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 26, 2013

    NIMEOLEWA NA MZUNGU.
    1. ANABADILISHA NEPI
    2. ANAMBEBA MTOTO KUMPELEKA DAY CARE
    3.ANAPIKA
    4.ANASAFISHA NYUMBA
    5.NIKISAFIRI ANA FANYA SHUGHULI ZOTE ZA NYUMBANI
    6. HAJAWAHI KUNIPIGA WALA KUNIKASHIFU
    7.NDUGU ZAKE HAWAJAZANI KWANGU
    JE KUNA MBONGO MWENYE SIFA HIZO?

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 26, 2013

      Ndio wapo. Ehe,swali la ziada?

      Delete
  15. AnonymousJuly 27, 2013

    Wewe unafikiri kazi ni kukaa ofisini tu. Hii ni kazi sawa na kazi nyingine ndiyo maana wenzetu wameendelea. Unamdharau anayefagia wakati analipwa mshahara kama wewe na hajaja kwako kukopa au kulia njaa?
    Nadhani unamatatizo na upeo wako ni mdogo sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...