WASANII mbalimbali wanaojitokeza katika Tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt
Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ linalofanyika
katika Uwanja wa Nyamagana, jijini hapa wamezua mambo kwa kutaka wapambanishwe
na wakongwe.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wasanii hao walisema wana uhakika mkubwa wa kuwafunika wakongwe na wanataka mpambano wa ‘live’ siku ya kufunga tamasha hilo hapo kesho.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wasanii hao walisema wana uhakika mkubwa wa kuwafunika wakongwe na wanataka mpambano wa ‘live’ siku ya kufunga tamasha hilo hapo kesho.
Akizungumza kwa
kujiamini, Paul Mabula ‘Bonge’ alisema msanii Jacob Steven ‘JB’ hawezi kutamba
kwake, kwani yeye anajiona ni mkali zaidi kuliko yeye na akikubali wachuane
‘live’ hapo kesho atafanya vitu vya ajabu vitakavyowashangaza wengi.
“Yule JB ni
bwa’mdogo tu kwangu, kama anajiamini mwambie Jumapili nipambane naye halafu
aone nani mkali, mimi najiamini mno katika kila kitu,” alisema Bonge kwa
kujiamini mno.
Isha Rama
ambaye mwenyewe anajiita Irene Uwoya, alimtaka msanii huyo pamoja na Jacqueline
Wolper wapambane naye, kwani anaweza kuwafunika wote wawili kwa wakati mmoja.
“Nitakuja na
dogo wangu hata yeye ana uwezo wa kumfunika (Vicent Kigosi) Ray na watatambua
Mwanza kuna vipaji vingi na vyenye uwezo zaidi kuliko wao,” alisema Isha.
Akizungumzia
hilo, Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, amefurahi kuona wasanii wa
Mwanza wanavyojiamini mno na kuwatahadharisha wakongwe wakae chonjo kesho kwa
upinzani mkubwa watakaoupata.
“Hapa Mwanza
tumeshuhudia vipaji vya kila aina, nimefurahi kwa kiasi kikubwa kwa jinsi
wanavyojiamini, kwetu Grand Malt tunaamini lengo letu limefanikiwa kwa kiasi
kikubwa,” alisema.
Mratibu wa
Tamasha hilo, Musa Kissoky, alisema naye amefurahishwa pia na wazo la wasanii
hao na kuwaonya wakongwe watakutana na vitu visivyo vya kawaida hiyo kesho.
“Hapa Mwanza
kuna balaa tupu, maana hawa wasanii sikutegemea kama wanajiamini kwa kiasi
kikubwa kama hivi, tutaona hiyo Jumapili mambo yatakavyokuwa,” alisema.
Tamasha la Filamu la Grand Malt lilianza rasmi mwishoni mwa wiki na linatarajiwa kumalizika kesho, huku wakati wote wa tamasha hilo zikionyeshwa filamu mbalimbali za Tanzania.
Tamasha hilo la
filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho
kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...