Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakitazama moja ya filamu iliyokuwa ikioneshwa jana usiku kwenye viwanja vya Nyamagana,ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Filamu ya wazi lililojulikana kwa jina la ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’.Tamasha hilo lilizinduliwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya na kusababisha shangwe tupu kwa wote waliokuwepo ndani ya uwanja huo.
Katika uzinduzi wa tamasha hilo,kuna burudani mbalimbali zikitolewa ikiwemo na wakazi wa Mwanza wenye vipaji vya kucheza na kuimba,walipewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kama ionekanavyo pichani,ambapo mwisho wa mashindano hayo kuna atakaeibuka na kitita cha shilingi laki mbili.
Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza jana kushuhudia muenedelezo wa tamasha la filamu,lijulikanalo kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ kwenye uwanja wa Nyamagana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...