Kamera ya Globu ya Jamii,mchana wa leo imeinasa taswira hii ya Mdau akiwa kaweka kishoka barabarani katika kijiji cha Mbwewe,Wilayani Handeni huku akiwa hana wasiwasi wowote kana kwamba kaweka kishoka hicho kwenye bombe moja la Shangingi huku magari kibao yakiendelea kupita kwenye barabara hiyo.Mdau unaionaje hii??
Home
Unlabelled
Umeona hii??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hamna NOMA mdau kujipumzisha
ReplyDeletealisikia katika taarifa za habari OBAMA yupo bongo,usafiri wake utakuwa juu kwa juu na maelikopta, barabara zote zimefungwa kwa magari,kama bongo yetu nchi huru, kapata siku mbili za kujisikia yupo katika barabara za utelezi kama gomba la ndizi, siku za kawaida hapakaliki maeneo hayo.
mikidadi mdau wa denmark
Haina taizo, kwanza amekaa ukingoni kabisa mwa barabara, gari itafuata nini huko? Pili amekaa kushoto, hivyo magari yanayokuja anayaona ikiwa atatokea dereva mlevi.
ReplyDeletehata mbuzi hawezi fanya hivyo. watanzania wamezidiwa akili na wanyama.
ReplyDeletegigo guy..
SIO MTU HUYO, HIO HANDENI MNAIJUA NINYI? MWAFIKIRI MTU HUYO SIO KABISA, MARA NYINGI HILO DUDE HUONEKANA HAPO! CHEZEA TANGA WEWE!
ReplyDeleteHali ya maisha inapokua ngumu watu hupoteza matumaini,mtu aliyepoteza matumaini uhai kwake hauna thamani tena,kuliona hili inataka weredi kidogo.Matukio mengi yenye kufanana na haya yanatokea na yatazidi kutokea huko nyumba kwa kasi hii tunayoenda nayo.
ReplyDeleteAmeghafilika in afilika.
ReplyDeleteAnyways...dogo amekaa kimachale, akiona namna gani..., "instinct" zitamrusha pembeni !
ReplyDeletekwa sisi wazoefu na wasafiri katika njia hizi napenda nitoe tahadhari kuwa wengine kama hawa wapo wakichagua gari za kuzisababishia ajali then wanaiiba. muwe macho sana. wapo hata usiku wa manane. wengine wanalala kama vile hawajitambui. ukilogwa ukasimama utaibiwa vitu.
ReplyDeletekama unaakili unajiuliza mtu mwenye afya njema kama hiyo anakaa barabarani kufanya nini?
Kwani kuna ubaya gani kum-beep Israel????
ReplyDelete