Na Abdulaziz Video,Lindi
Huku kukiwa na zaidi ya sh milioni 700 zikiwa zimeanza kutumika katika ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi ambapo zoezi la ujenzi wa kituo kipya cha mabasi wilayani humo kuanza kujengwa na kutumika katika maeneo ya uwanja wa ndege,Baadhi ya Abiria leo wametishia kugoma kutokana na Kuzuia tena uwepo wa kituo cha karibu na maeneo ya Mjini kutokana na Umbali uliopo na kituo hicho kipya.

Hali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya baadhi ya Abiria kugomea kituo hicho kipya kutokana na Halmashauri ya Wilaya hiyo kushirikiana na Jeshi la
Polisi kufuta kituo cha Tunduru na kuagiza wasafirishaji wote
kutumia kituo cha Stesheni kuwa cha mwisho njiani kabla ya kufika kituo
kikuu ambapo kuna umbali mrefu hali inayofanya Abiria wengi kunufaisha
watoa huduma za bajaj na Bodaboda huku wengine wakitembea Umbali Mrefu
kwa kukipita msituni.
Akiongea na Mtandao huu Mwandishi wa Gazeti la Raia Mwema wilayani
humo,Ahmaid Mmow alieleza kuwa hali hiyo imeleta kero kubwa kwa Abiria
wanaosafiri kati ya Nachingwea,Masasi,Newala,Lindi na Dar es salam
huku wengine wakisafiri wakiwa na shida mbalimbali za kijamii.
Abiria wengi baada ya kuanza kwa stand mpya waliumia sana na umbali na
msitu uliopo lakini Halmashauri ilipoanzisha kituo cha Tunduru ya Leo
kidogo kilileta ahueni sasa sijui ni kwa nini wamekifuta hali
inayofanya abiria wengi kulazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya
km 5 hadi stand Mpya na stesheni.
Hii inaumiza sana hasa wenye wagonjwa,Kufuatia hali hiyo Baadhi ya Mawakala wa Mabasi ya Abiria na Abiria
wamedhamiria kuitisha maandamano ya kuhamasisha kutotumia kituo kipya
kinachoendelea kujengwa hadi kitakapokamilika kutokana na kukosekana
kwa baadhi ya huduma muhimu za kijamii ikiwemo mabanda ya kupumzikia
Abiria.
Basi zikiwa stendi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...