Nyota wa mchezo wa mpira wa miguu wa
Marekani(American Football) Rays Lewis akimpa
RaisDkt. Jakaya Kikwete zawadi ya kofia yenye nembo ya timu yake wakati
nyota huyo alipomtembelea Rais Kikwete mjini Arusha.Nyota huyo yuko nchini
ambapo ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa huduma kwa wagonjwa wenye ulemavu wa
kusikia inayotolewa na taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini
Marekani.Wagonjwa zaidi ya 3500 wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo
inayotolewa bure na taasisi hiyo.
Muasisi wa Taasisi ya Strakey Hearing
Foundation Bwana Bill Austin Starkey
akimhudumia mtoto Lissa Frank(9) ambaye alikuwa kiziwi tangu kuzaliwa na kuweza
kusikia baada ya kupata tiba na huduma ya kuwekewa kifaa maalumu katika kliniki
maalumu iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mkoani Arusha leo.
Waasisi wa Taasisi ya Starkey Foundation Bwana Bill
Austin Starkey(kulia aliyeinama) na Mkewe Tani Austin(Wapili kushoto) pamoja na
mhudumu kutoka hospitali ya Seliani(kushoto) wakifurahi baada ya mtoto Lissa
Frank(9) kuweza kusikia vyema baada ya kupatiwa matibabu katika kliniki maalumu
iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mjini Arusha leo(picha na Freddy Maro)
====== ===== =========
WALEMAVU WA KUSIKIA WANUFAIKA NA HUDUMA ILIYOTOLEWA NA
TAASISI YA STARKEY HEARING FOUNDATION.
Na.Freddy Maro,Seliani Arusha.
Julai, 7 ,2013.
Zaidi ya Watanzania 3500 wenye maradhi ya kusikia
wanatarajiwa kunufaika kwa huduma ya tiba inayotolewa na Taasisi ya Starkey
Hearing Foundation yenye makao yake jijini Washington nchini Marekani.
Muasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing foundation Bwana Bill Austin Starkey ameyasema hayo wakati wa kliniki
maalumu ya kuwatibu watu wenye maradhi mbalimbali ya kusikia iliyokuwa
ikifanyika Katika hospitali ya Seliani mjini Arusha baada ya kutoa huduma hiyo
katika miji ya Dar es Salaam na Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Nimefurahishwa sana na kutiwa moyo kwa kazi tuliyoifanya
ya kuwahudumia watu na kuwawezesha kusikia ambapo wengine ndiyo wameweza
kusikia kwa mara ya kwanza tangu walipozaliwa.Furaha yao ni kitu cha kutia moyo
sana katika juhudi zetu.Madaktari wa kitanzania tulioshirikiana nao wamefanya
kazi kubwa na nzuri” alisema Bwana Starkey ambaye ameambatana na timu ya wataalamu
na watu mashuhuri kutoka nchini Marekani ambao wametoa misaada mbalimbali
kugharamia kampeni hiyo.
Bwana Starkey amesema kuwa watu wengi walijitokeza wakati
wa kliniki hiyo maalumu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuongeza kuwa
katika siku tatu walizokuwa mjini Arusha wagonjwa zaidi ya 600 walipatiwa
huduma hiyo ya matibabu kwa kuwekewa
vifaa maalumu katika masikio yako na kuwawezesha kusikia vyema na kusema kila
mwaka shirika lake litafanya mipango ya kuhakikisha kwamba huduma hiyo inakuwa
endelevu.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wazazi wenye furaha
baada ya kuona watoto wao wenye umri kati ya miaka mitano na kumi wakiweza
kusikia vyema kwa mara ya kwanza katika maisha yao baada ya kupatiwa matibabu kwa kuwekewa vifaa
maalumu katika masikio yao huduma ambayo imetolewa bure na shirika hilo na
isingekuwa rahisi kuipata kwa watu wengi walio na kipato cha chini.
Bwana Bill Austin Starkey aliwashukuru wafadhili
mbalimbali waliowezesha mpango huo wa matibabu kufanikiwa na kuongeza kuwa falsafa ya taasisi yake ni
“Ili Dunia ipate kusikia” imeweza kutekelezwa kwa vitendo kwa sababu anaamini kuwa kukiwa na nia ya dhat na moyo
wa kushirikiana kutekeleza jambo fulani mafanikio ni bayana na mabadiliko mengi
chanya yatawezekana katika ulimwengu.
Bill Austin Starkey na mkewe Tani Austin ambaye ni muasisi mwenza
wa taasisi hiyo pamoja na washirika wao wanatarajia kwenda nchini Malawi kutoa
huduma kama hiyo na baadaye kurejea tena nchini kutoa huduma kabla ya kuondoka kurejea nchini marekani.
Mmoja wa wataalamu wanaotoa huduma katika kliniki
hiyoDkt. Ron Brouillete alisema mbali na kuzaliwa na ulemavu wa kutosikia
wangojwa wengine waliotibiwa katika kliniki hiyo walipata madhara ya kutosikia
kutokana na matumizi holela ya dawa ya kutibu Malaria aina ya Quinine.
“Napenda kutoa ushauri kwa madaktari na wahudumu katika
sekta ya afya kuepuka kuwapa dawa ya Quinine wagonjwa wa Malaria.Dawa hii
itumike kwa uangalifu mkubwa na pale ambapo dawa nyingine zimeshindwa kumtibu
Mgonjwa,” alisisitiza mtaalamu huyo kutoka nchini Marekani .
Mmoja wa wafadhili wa mradi huo anayefuatana na Bwana
Bill Austin Starkey ni mcheza mpira wa
miguu maarufu wa Marekani(American Professional Football) Bwana Ray Lewis
ambaye pia anachezea ligi ya taifa ya mpira wa miguu ya nchi hiyo(National
Football League).
Awali Mchezaji huyo alimtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete aliyekuwa mapumzikoni mjini Arusha na kusema kuwa Rais Kikwete ni mmoja
kati ya viongozi mashuhuri barani Afrika wenye maono ya mbali na nia ya dhati
ya kuwahudumia wananchi wake.
“Nimesoma habari nyingi mambo mangi yenye mafanikio
makubwa anayoyafanya Rais Kikwete na nilipopata fursa ya kuja nchini Tanzania
nikatumia nafasi hiyo kuja kumsalimia,kumsikiliza na kumpongeza.Ni mtu
mnyenyekevu sana na nimefurahi sana kumtembelea na kuongea naye,” alisema nyota
huyo wa mpira wa miguu Marekani muda mfupi baada ya kukutana na Rais Kikwete
ambapo alimzawadia kofia yenye nembo ya timu yake.
Bill Austin Starkey na mkewe Tani Austin waliunda Taasisi
ya Starkey Hearing foundation mwaka 1984 kwa lengo la kusaidia watu wenye
maradhi ya kusikia na mpaka sasa maelfu ya watu katika sehemu mbalimbali
duniani wamenufaika na huduma inayotolewa na taasisi hiyo.
Ray Lewis ndani ya bongo siyo mchezo !! GO Ravens Go ! Baltimore all day!! the super bowl champ 2013....
ReplyDeleteHapo kikwete yupo na Miraji? Ray Lewis amefanana na Miraji.
ReplyDelete