Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2013

    Mtangazaji unaousena "..mtaa wa Fairmont stree.." au "chuo kikuu cha Howard University.." unajidhalilisha wewe binafsi pamoja na taaluma yako (kama ulisomea utangazaji)

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2013

    Hii kali. Sijawahi kusikia TV broadcasters wa nyumbani wakisema "Chuo kikuu cha Dar-es- Salaam University" wala "mtaa wa Azikiwe street" Nakushauri mtangazaji uchukue application forms hapo Howard university ili kurekebisha taaluma yako angalau ufanane na watangazaji wenzio.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2013

    Inawezekana kukuwa na makosa ya kibinadamu ktk kufikisha ujumbe huo lakin kuna njia bora zaidi zaidi za kumfikishia mtangazaji kuliko nae kumdhalilisha.

    Ukiangalia message aliokusudia mtangazaji kuifikisha kwa watazamaji amefanikiwa kufanya hivyo pengine kwa asilimia 80 tungejaribu kua positive.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2013

    Sina kawaida ya kutoa maoni lakini kwa hili naomba na mimi nichangie, hususan baada ya kuguswa na maoni hayo ya juu kuhusu mtaa na university kutajwa mara mbili kwa lugha tofauti, a. Ila kwanza lazima nikiri kuwa na maslahi nayo (declare interest), kwani sina tatizo na hicho kitu, baada ya kukizoea kutoka kwa Anko Michuzi ambaye amekuwa akikitumia sana na sie wenyeji wa blogu yake ya jamii tushazoea kukisikia maana naye hutumia misemo hiyo katika kunogesha Libeneke.

    Maoni yangu hayahusu mjadala uliopo hapa ya kufanya ama kutaja kitu kimoja kwa kutumia maneno mawili yanayofananan (kwa kizungu tautology, kama sikosehi, yaani the use of redundant words).

    Nia yangu hasa ni kusemea huu ugonjwa wa Watanzania wa kuwa wajuaji wa kila kitu, wepesi wa kushabikia makosa ya wenzao na kubwa kuliko yote, kukatishana tamaa.

    Watanzania tungekuwa mbali sana endapo tungepiga vita kaugonjwa hako, maana kanarudisha mno maendeleo ya nchi na watu wake.

    Iwe mashuleni, makazini, sehemu za starehe na hata nyumbani, Watanzania ni hodari sana kuvutana mashati na kuona makosa ya wenzao huku wakiwa vipofu wa makosa wayafanyayo wao.

    Utakuta mtu anataka kusoma kwa bidii, ama kufanya kazi kwa bidii na uaminifu na kwa uwezo wake wote, ama kuwa mtoto ama mtu mzuri nyumbani, lakini adhabalabu utakuta wenzie wanamuona fala, mstaka sifa, hafai ama anajipendekeza, wakati wao huo huo hawafanyi lolote la maana. Raha yao wao ni kuona huyo anayejutuma ama anayejitahidi aache ili awe kama wao. Mfano wake mkubwa ni huo wa wanaomponda Alex, ambaye ameibuka na kuanza kusaka na kumwaga habari kwa weledi unaotakiwa, lakimni tayari Waswahili wanaacha yoooote mazuri na kuanza kutoboa mabaya. Mwishowe utakuta wanataka Alex abaki kama wao.

    Najua naongea nini, na sio kwamba sijaona TAUTOLOGY katika wa Alex katika kutaja majina ya mtaa na chuo, la hasha. Nimeyaona na kusikia vizuri tu, ila hao wajuaji wajue wana hako kaugonjwa ambako wanatakiwa waondokane nako. La sivyo watabakia MANUNGAYEMBE kama walivyo Watanzania wengi.

    Kaka Alex achana nao hao. Kumbuka kwamba mti wenye matunda ndio unaotupiwa mawe. Hivyo kama hao jamaa wanaougua ugonjwa wa kurudishana nyuma wamesikia hayo wanayodai ni makosa, ujue wanakuhusudu ilam hawataki usonge mbele.

    Piga mzigo wewe na wenzio, maana mnaleta mapinduzi katika habari za Kiswahili huku ughaibuni. Mimi na familia yangu tu mashabiki wakubwa wa Swahili TV. Achana nao hao MANUNGAYEMBE, tuoe raha.

    Na wala suishangae kukuta wao ama wagomnjwa wengine wa Inda wananijibu kwa kejeli na matusi. Ndio kawaida yao...Pia watu walioenda shule huwa hawakosoi mambo madogo madogo kama hayo. Ukiona hivyo wao ndio ngumbaru.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2013

    Well said anony hapo juuu....wasomaji wa michuzi wa long time mbona tumezoea lugha yetu ya Daraja la Salender bridge, Mtaa wa Congo street. nk

    hawa jamaa wakisiki ile " my wife wake" watasemaje?

    Subiri wajuaji wa comment ndo ulete zako.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2013

    Mtangazaji anaongea utafikiri anakimbizwa. Control breathing yako, kijana.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2013

    Ankal Michuzi anapotumia neon moja kwa lugha mbili tofauti huwa anafanya hivyo ki-utani na utani wake unaishia kwenye blog yake tu, siyo kwenye TV. Sidhani kama huyu mtangazaji alikuwa anatania watazamaji wake na watu msibani. Wadau mnaomtetea naomba mseme kama makosa haya mmewahi kuyasikia kwa TV broadcasters wa nyumbani akiwemo Michuzi. Tunapomkosoa huyu mtangazaji 'fake' tunamsaidia ili asiendelee kujidhalilisha na kutudhalilisha watumiaji wa lugha ya Kiswahili. Wakosoaji tuna lengo la kumsaidia na siyo kumdhalilisha maana tayari ameshjidhalilisha yeye mwenyewe.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2013

    Lazima akosolewe.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2013

    Tumsaidie,kwani pia kiingerza kibovu sana sana na kama kuna nafai ajilemish ama sivyo ni kujidhalilisha na kulidhalilisha taifa

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2013

    Mtangazaji anapumua utadhani anakimbizwa na samba. Sijui anaogopa nini. Take a dip breath and relax boy. Haya ndo matatizo ya kuvamia taaluma za watu bila kuwa na ujuzi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 15, 2013

    Audience ya mtangazaji ni Marekani amewapa tu video hii muone kuna Swahili TV, anawaelimisha wazungu kwa lugha mbili, ndio anapenyeza kiswahili waelewe. Ujumbe mtangazaji aliokusudia kuufikisha kafanikiwa kwa 100%. Hata CNN huwa wanakosea sometimes. Kikubwa jamaa kaanzisha Swahili TV anawaletea habari hilo ndio lengo. Kwa mara ya kwanza ameripoti toka mtaani inabidi mkubali kwa hilo. Badala ya kukaa nyuma za computer zenu mkijificha kama ma-anony na kuponda. Hakuna mtanzania aliyeanzisha TV marekani.Mtaendelea kuponda mkimaliza shida zenu ziko pale pale, mwenzenu anaendelea. Kama hutaki kuangalia Swahili TV hujalazimishwa acha kaangalie vitu vingine au anzisha na wewe TV yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...