MBUNGE wa Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Saidi Mwanamdogo, akizungumza na wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanambwewe waishio Dar es Salaam (MNDF), leo katika ukumbi wa Shule ya Msingi Ali Hassani Mwinyi, mjini Dar es Salaam. Wanachama hao walimwalika kwenye kikao chao cha kujadili jinsi ya kuuendesha mfuko huo kwa manufaa ya wananchi wengi.
Katibu wa wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya wanamtandao wa Mbwewe waishio Dar es Salaam, Hassani Msonde akizungumza mwanzoni mwa kikao
Mwenyekiti wa Umoja huo, Rajabu Papa akifungua kikao hicho
Mjumbe wa Kamati ya Umoja huo, Fatuma Kikwappe akisoma risala huku viongozi wakimsikiliza kwa makini akiwemo Mbunge Bwanamdogo.
Kisha akaikabidhi risala hiyo kwa Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo
Mbunge Saidi Mwanamdogo akiwakabidhi dola za Marekani, viongozi wa umoja huo, ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kufanikisha usajili.
Mwenyekiti akimkabidi Mbunge Katiba ya Umoja. NA theNkoromo Blog
Je huu tunaonyesha mfano gani toka kwa viongozi wetu kutumia dola za marekani badala ya shillingi ya tanzania?
ReplyDeleteDola kwa ajili ya nini? inamaana siku hizi wabunge wanatembea na dola badala ya Tshs?
ReplyDeleteNi hatari kweli kweli! Au kuwaonyesha hao Wanambwewe kuwa anazo? Shame to you Mwanamdogo.
kwa kweli mheshimiwa ameboa sana,na hizo dola zake ambazo hata mia hazifiki,tunajua kwamba wanamiliki account za dola,lakini hajui yalipo maduka ya kubadili pesa?kikao cheyewe cha kawaida tu anapeleka hela za kigeni, tena kiduchu, mbona tunaona michango mikubwa watu wanatoa hela za madafu tena za kutosha.Ahamie kwa Mugabe wanakotumia dola kama anaona madafu yamechomsha.kweli hawa waheshimiwa wetu wana tofauti sana na sis tuliowapa 'kula'
ReplyDeleteWadau Mkubwa Mhe. mbunge ametumia DOLA ZA OBAMA ili aweze kufanya Usajili wa Dirisha Dogo ili aweze kutokea hapo kwa kutoa lawama kwa kuwa kama mnavyoona Dola zenyewe masifuri yake yapo chini ni 20 na za 50 mbili tatu hivi Kiasi cha kama hata Laki haifiki!!!
ReplyDeleteSi mnajua tena?
Apew e Taarifa Prof. Ndulu Gavana wa Benki Kuu.
ReplyDeleteHili noi mojawapo la Kosa la Kibenki kwa kuwa ktk Moja ya ''CENTRAL BANK MONETARY POLICY INSTRUMENTS'' yaani Sera Kuu za Benki Kuu ni MORAL SUATION yaani KUWAPA MWAMKO WANANCHI hasa ktk Suala la kutumia Sarafu ya Ndani ya nchi ktk manunuzi na mzunguko wa matumizi ya kawaida wakiwa ndani ya nchi.
Ina maana hata Mgeni akishaingia Tanzania anatakiwa abadili Fedha zake akiwa Uwanja wa Ndege ili aweze kufanya matumizi yake kwa Fedha za ndani akiwa nchini hadi siku akiondoka ndio alizobaki nazo atazibadili kuwa Dola akiwa Uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kurudi kwao.
Benki Kuu ilishatoa angaizo mara kadhaa ni vile Amri hizi hazitekelezwi, mfano nchini Rwanda ukiwa Mjini Kigali ukitumia Dola ama Fedha za Kigeni unakamatwa!