Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu hawa, wanaoonekana katika hizo picha hapo chini, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vikubwa vya kihalifu hapa nchini na katika maeneo mbalimbali nje ya nchi yetu.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yetu, kutoa taarifa za watu hawa popote watakapoonekana katika kituo chochote cha Polisi kilicho caribú, ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkondo wa sheria.
Ndugu mwananchi, hata kama ni ndugu yako, usisite kutoa taarifa za watu hawa kwa sababu ni watu hatari sana. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa watu hao.
Kwa taarifa unaweza pia kupiga Makao Makuu ya Polisi kwa kutumia simu namba 0754 78 55 57.
Imetolewa na:-
Advera Senso - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)


.png)


Mbona ukachero wenyewe uchwala! kawaida unatoa majina ya hawa majangili, umri wao, urefu,wapi wanaishi, wapi wanapendelea kupoteza muda, alias wanazotumia, na sema donge nono la kiasi ganI?
ReplyDeletehapa washinwa kurudisha mgao
ReplyDeleteNimewaza hivyo hi yo. Itakua walikiuka masharti ya kupeleka asilimia fulani ya mapato kama walivyokubaliana.
Deletewanaitwa akinanani
ReplyDeleteKweli hata kama ni ndugu yako, vinginevto unaweza ukafuga nyoka, atakuja kukung'ata mwenyewe,
ReplyDeletehttp://miram3.blogspot.com/2013/07/wema-hauzo-27.html....pitia ujumbe huu hapa:
ni watu hatari sana,wamefanya nini?ni akina nani?more details watu waelewe.
ReplyDeleteKwa makosa gani hasa? Mkisema angalau aina ya uhalifu ni rahisi zaidi kuwapata maana watu watajua nini cha kuangalia au kuweka tahadhari katika maeneo mbalimbali. Pia mkitaja majina wanayojulikana kwayo...hata kama ni feki na wanayabadili itasaidia. Jamani ndugu zetu mbona mnatoa habari nusu nusu? Na zawadi nono ni kiasi gani?
ReplyDeleteHivi wewe msemaji wa jeshi la polisi kabla ya kutoa taarifa hii na kuoomba msaada kwa wananchi haukuweza hata kidogo kutafuta ushahuri wa kitaalamu wa jinsi ya kuandika taarifa kama hii ? Acheni usanii kazin...Tupeni sisi walengwa taaarifa kamili za hawa wanaosadikiwa kuwa wahalifu...km vile umri,maumbile yao, matembezi yao, wanatoka mikoa ipi ...Tufanye kazi kitaalamu jamani..kama hamkuwa tayari na ripoti kamili za hawa watu ni bora mngekaa kimya tu kuliko kujiabisha hivyo...na hilo donge nono ni kiasi ganiiiii ?
ReplyDeleteWatajwe Majina kwa uchache:
ReplyDeletePia ni vema watolewe taarifa zao wanapendelea kuwa maeneo gani?
Tupo tayari kutoa ushirikiano kwa maslahi ya nchi na ustawi wa jamii yetu ya Tanzania.
Tangazo la kibolizozo kweli,
ReplyDeleteHata kama ni ndugu yangu sisemi NG'O, maana hamjasema zawadi ni kiasi gani,
Kazi kwenu.
Huo ndio weredi wa jeshi letu la polisi jamii,tuwape ushirikiano wetu jamani angalau kwa kutoa maoni yetu kwa blog kama hii.
ReplyDeleteMajina:
ReplyDeleteWa kwanza anaitwa Nyanya tamu
Wa pili Muhogo mchungu
Wa tatu Pilipili chachu.