Ndugu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,

Napenda nichukue fursa hii kuwajulisha rasmi kwamba Nchi yetu imepata heshima ya kutembelewa na Waziri Mkuu wa Thailand ambaye atawasili Nchini tarehe 30/07/2013. Ziara hii ni ya kikazi (state visit) na atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere majira ya saa 6:30 mchana na kulakiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais wetu mpendwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa.

Ndugu Wananchi,
Baada ya kuwasili Mhe. Waziri Mkuu wa Thailand atakagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na pia atapata fursa ya kukagua vikundi mbalimbali vya ngoma ambavyo vitakuwa vikitumbuiza na kutoa burudani kwa Mgeni wetu na msafara wake.

Ndugu Wananchi,
Mgeni wetu baada ya kukagua vikundi vya ngoma na burudani ataondoka kuelekea Ikulu kupitia barabara ya Nyerere, Railway, Gerezani, Sokoine Drive hadi Ikulu. Akiwa Ikulu atasaini mikataba mbalimbali kati ya Serikali ya Tanzania na Thailand. Usiku atashiriki katika dhifa maalumu iliyoandaliwa na Mwenyeji wake.

Ndugu Wananchi,
Tunaomba radhi kwamba barabara hizi nilizozitaja zitafungwa kwa muda kupisha misafara ya Viongozi wetu Wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere kumlaki Mgeni wetu hususan barabara ya Nyerere kuanzia saa 6.00 mchana hadi saa 7.30 mchana.

Ndugu Wananchi,
Tarehe 31/07/2013 Waziri Mkuu wa Thailand atatembelea Mbuga za Wanyama za Serengeti.Tarehe 01/08/2013 atarejea Dar es Salaam na kuagwa rasmi katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere na kuendelea na ziara yake huko Uganda.

Ndugu Wananchi,
Kama ilivyo ada tunaombwa kumlaki mgeni wetu kwa shangwe na bashasha katika maeneo yote atakayopita. Asanteni kwa kunisikiliza.

Saidi Meck Sadiki
MKUU WA MKOA

DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2013

    VIPI KWA HUYU HATUSAFISHI JIJI JAMANI?? HUU NI UJUMBE MZITO SANA TANZANIA.

    KILIMO KWANZA CHA MPUNGA HAPA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2013

    hii kaandikiwa bw Sadick, siyo kawaida yake, mhe; huyu kuwa na lugha za kistaarabu kama hii taarifa inavyojieleza, pengine kapata washauri wazuri, safari hii
    asante

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2013

    Shonawatra wa Obama welcome

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2013

    Vp ulinzi wake kama wa mh Obama? Je,ombaomba nao wameondolewa katikati ya jiji?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2013

    what a stunning beauty model pm, alex bura dar!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2013

    Uwanja wa Ndege wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere upo wapi? au ndo ule wa JKNA uliopo jijini DSM umebadilishwa jina?

    Mwisho tuna mkaribisha kwa mikono miwili mgeni wetu Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Thailand.

    Mdau
    Gogo-la-Mboto-Mwisho-wa-Lami

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...