Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akifunua kitambaa kuashiria Ufunguzi rasmi wa Hospitali Mpya ya Wilaya ya Namtumbo,Mkoani Ruvuma uliofanyika mchana wa leo,ikiwa ni sehemu za Ziara yake ya Kikazi katika Mkoa wa Ruvuma.Mbali ya Ufunguzi wa Hospitali hiyo Mpya,Waziri Mkuu amezindua pia Machinjia Mapya na ya Kisasa kabisa katika Wilaya hiyo ya Namtumbo pamoja na Kuzindua Mtambo wa Kufua Umeme katika Wilaya hiyo.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda (wa pili kulia) akipatiwa Maelezo machache juu ya Hospitali hiyo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa huo wa Ruvuma wakati akikagua Jengo la Hospitali hiyo.
Waziri Mkuu na Ujumbe wake wakiendelea na Ukaguzi wa Jengo la Hospitali hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh. Abdul Lutavi akisoma taarifa ya Miradi mbali mbali ya Maendeleo mbele ya Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda ambaye leo alikuwa Wilaya hiyo kwa ziara yake ya kikazi.
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mkoani Ruvuma,Mh. Vitta Kawawa akizungumza machache.kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Stephen Massele.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda kuongea na Wananchi wa Wilaya ya Namtumbo.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Brigedi ya Kusini,Brigedia Jenerali,John Chacha wakati alipokuwa akiwasili Wilayani Namtumbo Mkoani Songea,mchana wa leo.Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo,Mh. Vitta Kawawa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Khadija Palangyo ambaye ni Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium,uliopo kwenye Kijiji Mkuju,Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh. Abdul Lutavi.
Brg Chacha amekwea angani sio mchezo.
ReplyDeleteHeheheh!
ReplyDeleteMdau wa Kwanza Brigedia John Chacha anamlaza macho akikesha bila usingizi Raisi wa Malawi Mama Joyce Banda.
Brigedia Chacha anaonyesha mikono inamwasha na ana gadhabu sana kuikabili Malawi.
Mhe. Raisi Jakaya Kikwete mwachie Afande Brg. Chacha angalau atwange Kombora moja tu, la Salamu kuelekea katitaki ya Ziwa Nyasa ili angalau afarijike kidogo!
Kule Sudan Darfur kwa nini tupoteze Majeshi yetu bure?
ReplyDeleteNafikiri tungerudisha Kikosi chetu ili kuikabili Malawi.
Malawi endeleeni na Madai yenu ya kijinga sisi Tanzania tutakacho fanya ni Kumruhusu Brg. John Chacha afanye kazi yake!