Ndugu David Shinganya wa Kampuni ya SGC INVESTMENTS LTD akikabidhi cheki ya Kwacha Milioni Nane (ZK 8,000,000.00) kwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma katika kuitikia wito wa wazo la baadhi ya Watanzania waishio nchini Zambia walilolitoa kuchangia ukarabati wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia. Hafla hiyo ya kukabidhi cheki ilifanyika hivi karibuni Ofisini kwa Balozi Mujuma ikishuhudiwa na Maafisa wawili


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2013

    Ankal Michuzi IMETOSHA...kama hata hela ya ukarabati haipo basi ni vyema ubalozi ukafungwa kuliko aibu hii ya kutembeza bakuli...ina maana ubalozi umeshindwa hata kukusanya visa fee, etc...yaani serikal imeshindwa hata hili?

    si lazima tuwe na ubalozi Zambia..ni hivi hata nchi zilizoendelea haziwek ubaloz kila mahali..tunaweza kuufunga na waliopo huko wakapata huduma za kibalozi Malawi.

    mdau
    canada

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2013

    Hivi kweli nchi yetu imefikia hapa? Yaani serikali hata aibu haioni. Mkusanye kodi mnunue mashangingi halafu bado tuchangie ujenzi wa Ubalozi. Huku ni kujidhalilisha. Samahani sana kwakweli....!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2013

    Uyo bwana aliyetoa huo mchango Nampa pole sana kwa kujipendekeza kwake sijuie anatafuta security ya 2015? Ivi anautajiri gani kushinda nchi ya Tanzania? kwa hela ipi? Weww serikali ya bongo ina mashangingi mpaka ya kupelekea kila motto shule na mama sokoni ndo imeshindwa kukarabati ubalozi wa Zambia! Mh brother iyo mchango ungewapa wahitaji yatima, wajane na ocan road hospital wagonjwa wakapewa mahitaji ungepata thawabu kwa Mungu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2013

    Tanzania tambarare!!!! wakati serikali inanunua majumba makubwa ya kifahari katika ulaya na kuyafanya balozi au makaazi ya maafisa wao, balozi zetu za nchi za afrika tunaomba mchango.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 26, 2013

    Ningelikuwa mimi ndie balozi wa hapo ningelikuwa na aibu mno sio tu kukubali mchango huo bali pia kupiga picha kama ushahidi kuwa serikali yetu haina uwezo wa kutunza majumba ya balozi zake. Aibuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...