Basi la Shining Star likitelemka mlima Kitonga bila kujali usalama barabarani
Na hii ni baada ya dakika tatu au tano na ikanusurika ajali ya USO kwa USO na basi nyingine. Hapo ni Kitonga vile vile, hawa madereva hawawajibishwi?
Basi namba T484 AXV la kampuni ya Hood number 61 Kama Kwenye Picha iki overtake hapo kitonga Leo Majira ya saa Saba mchana na baada ya dakika tatu basi nyingine hapo juu ilifnaya kitendo kile kile na kunusurika ajali USO kwa USO na basi nyingine Hapa ni kitonga
Mimi nafikiri tuwe wazalendo ktk kutetea uhai wa binadamu na ktk mambo kama haya ni vyema hatua kali za kisheria zikaanzia kuchukuliwa kupitia picha kama hizi .1 mmiliki wa vyombo husika kama hayo mabasi ya abiria hapo pichani ajulishwe mara moja kuwa bgari lake limeonekana kama kupitia blog au oicha ya mwandishi au chanzo cha habari flani kikivunja sheria za barabara mda flani, sehemu flani, so mmiliki wa chombo husika akibanwa atamjua tu ni dereva wake yupi anahusika. 2 Wakati sasa umefika wa kuwachukulia sheria kali madereva wa aina hii ikiwezekana dereva wa aina hii anyang'anye leseni, na afungiwe maisha kuendesha chombo chochote cha moto na afungwe jela miaka mitano na faini juu nafikiri tukiwa siriasi na hivi vitu vitakua adabu nzuri na fundisho kwa jamii, mdau nawakilisha maoni yangu. Nawaomba wengine wenye uelewa tusaidiane ktk hoja juu ya mambo kama haya
ReplyDeleteHivi kwa picha kama hizi tu kutoka kwa raia iweje Polisi wasifanye lolote? Nchi gani tunaijenga? Tunasubiri watu wafe na kukimbia kutoa misaada tu! Hao abiria hapo wote ni maiti watarjiwa! Inazuilika. Namba hizo zikamatwe na askari watangaze hatua zilizochukuliwa. Vinginevyo watu wanakosa imani na vyombo vya Serikali!
ReplyDeleteKweli maderava wanalicence halali? Wako wapi waajiri wao. Inaogopesha lakini abiria nao wameshonwa midomo?
ReplyDeletekwa kweli hii ni hatari sana,na ndiyo tabia ya madereva wa mabasi hasa njia ya Iringa.Nilishapendekeza tena sheria ibadilishwa,dereva anapopata ajali na ikasababisha kifo au vifo,kwa uzembe, ahukumiwe kama mtu mwingine aliyeua,hapo ndipo madereva wataheshimu maisha ya watu (pengine,sijui maana ni kama wamechoka na maisha na wanatamani sana kufa kwa hiyo huenda isisaidie)
ReplyDeleteSakata la mafuta ya ubuyu, waziri mwenye dhamana ya afya amesema anawaachia wananchi wenyewe waamue kutumia au kuacha,Pengine hata haya magari ambayo kila uchao tunaoneshwa hapa yakivunja sheria waziwazi tena wakati mwengine mbele ya askari wenda ikawa wakubwa/wahusika wameshakata tamaa na kuamua kuwaacha.
ReplyDeleteNashangaa mwizi wa kuku hupigwa mpaka kufa au akapelekwa jera lakini hii mijinga iliyo jazana humo ndani ya hilo basi yote yanaona kwa mimacho yao kwamba DEREVA anataka kuwauwa kwa makusudi ndo kwanza inakenua mimeno,,nakuamsheni kwenye usingizi mzito nyie wehu na wajinga DEREVA kama huyo mnampa kipigo cha hali ya juu na ikiwezekana mmalizeni kabisa,,njia ya kummaliza au kumpa kipigo cha hali ya juu ni hii hapa, mkigundua DEREVA anavunja sheria za barabarani kama vile MWENDO kasi au kuwapita wenzake kwenye kona pasipo kuona mbele,,kwa hiyo mnachotakiwa kufanya nyie abiria wote ndani ya basi ni kuambizana kimya kimya kisha mmoja wenu ajifanye anataka kwenda kuchimba mti au kwaluga nyingine kushikwa na haja kubwa au ndogo, lazima DEREVA atasimama ndio hapo mnaanza kumchomoa pale alipo,chapa yeye maliza yeye au akizinduka ajikute yopo hosipital ya TAIFA, hiyo ndio dawa yao MADEREVA WAJINGA au WAZEMBE mkitegemea polisi mtamalizika WATANZANIA amkeni jilindeni wenyewe,,mm mwenzenu yalinikuta mwizi kaniibia nimempeleka polisi kaachiwa akaanza kujigamba na kunitishia maisha lakini alijuta kuzaliwa nimemla ULODA kilazima mwenyewe kahama kimyakimya,naitwa kisiki cha mpingo,naijua sheria napia naiheshimu ila ukijifanya mjuaji zaidi nakuchenjia kibao, 1 luv my people.
ReplyDeletemdau uliyesema abiria wamefungwa mdomo, mie sikusapoti mana abiria hawana usukani, anayeamua speed ya basi na overtake ni mwenye usukani tu! Abiria hata waongee hiasaidii bali sharia ichukue mkondo wake na adhabu kali zitolewe kama wadau waliotangulia walivyosuggest. Abiria wengine labda wamelala wamechoka na pilika zao, huwezi kumfanya abiria awe dreva at the same time! Tufikirie kabla ya kuandika...! Au ungekuwemo kwenye basi ungemtoa dreva ukaendesha wewe hapo? unayesema abiria hawana midomo. Watz wanapenda kelele jamani!
ReplyDeletePolisi huwa wamewekwa 'mifukoni' na hawa madereva kwa tshs 2,000/= hawa dawa hayo kuwapeleka SUMATRA
ReplyDeletehakuna hatari yoyote mimi ni msafiri na dereva wa masafa ya huko mbeya iringa songea na sehenu nyingine, hapo ukiwa hujawahi kuendesha gari huko unaweza leta ajari, lakini kwa wazoefu huwa wanaangalia kwa mbele na kuona kama kuna gari au la ? na pia lazima ujue kuwa mtu anaepandisha ndio anatakiwa kupishwa na unaeshusha unatakiwa kumpisha apandae. acheni majungu
ReplyDeleteTatizo, Sheria za usalama barabarani Tanzania nyingi zinakusanya mapato tu, case kama hizi anaitwa mmiliki au linakamatwa gari halafu mmiliki anatozwa faini, wakati mtenda kosa ni dereva, kosa kafanya dereva adhabu kapewa mmiliki je dereva atajirekebisha? MAONI Dereva akikiuka sheria ashushwe kwa ajili ya kuadhibiwa yeye, mmiliki ataarifiwe ili alete dereva mwingine atayefuata sheria. ikiwa hivyo, mmiliki hatoajili dereva asiye na uhakika nae katika kufuata sheria, abiria hawatakubali dereva aendeshe hovyohovyo wakihofia kucheleweshwa safari pindi dereva akikamatwa na madereva wa aina hiyo hawatapata ajira
ReplyDeleteTatizo leseni wamezipatia bar... hawajui kusoma wala kuandika...lami zimewekwa hivi karibuni hao madereva hawajui maana ya mstari mweupe barabarani wala maana ya double yellow line.....abiria nao wakiona basi linakwenda kasi wanasherehekea hiyo nchi mmmm bado sana sijui tutafika lini tuendako.
ReplyDeleteNi kama vile watu hawajui pa kulalamikia matokeo yk kila abiria kimyakimya kivyake analalamika. Mi nliwahi kumtozesha faini kubwa konda wa basi la Tanga, kanipita hovyo, kalazimisha kurudi site yangu ili akwepe ajali AF akanipa cha 'kati', nkawahi kibaha stendi taarifu trafiki polisi ile anaingia akakuta risiti inamsubiri, 60000 , kwa kuovateki na ya kidole cha kati
ReplyDeleteSisi wenyewe pia abiria kama tunaona wahusika hawachukui hatua basi tukiona dereva anafanya ujinga tumtulize pembeni alafu tumchapeee mpaka akome nadhani itakuwa fundisho kwa madereva wapumbavu, sio tunakubali vifo Tu.
ReplyDelete