Bundi wa Ras Makunja hawana ukorofi na mtu, anadai Kamanda wa FFU Ughaibuni Ras Makunja.  Baada ya kujichukulia tuzo ya kimataifa ya bendi bora ya kiafrika barani ulaya,mkuu wa kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU kamanda Ras Makunja alikutwa akicheza na bundi wake katika makao yake "Anunnaki Empire" na alipoulizwa kulikoni awapende bundi hao na kwanini asifuge ndege kama kasuku ? Kamanda Ras Makunja alijibu eti "Bundi wake" hawana ukorofi na mtu ni ndege wenye upendo tu tena watulivu kuliko Kasuku. Kamanda Ras Makunja amedai kasuku wana kelele sana..lakini Bundi wakimya na wapole. Alipoendelea kuhojiwa akaamua kuuchuna.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Makunjas umejibu Vizuri sana!

    Nikiwa kama Mwana ndugu ktk familia yetu hii ya kuwakingia kifua Bundi ningependa uwaeleze Wajerumani sababu zingine hizi za ziada ni kwa nini ufuge Bundi badala ya ndege wengine?

    Ni hivi waeleze haya Matano (5),

    1.Ni njia ya kutoa mafunzo ya kujali viumbe na sio kwa maslahi kama kutarajia kuwachinja viumbe kwa vitoweo, Pana kila sababu ya kuwafundisha Binaadamu kuacha hulka mbaya saaana ya uchu kwa kufunga ndege au mifugo inayoliwa tu huku wakikwepa kufuga mifugo mingine mfano ndege kama hawa Bindi.

    2.Bundi wamekuwa wakitengwa sana zaidi ya ndege wengine.

    3.Ni somo kuifundisha Dunia jinsi ya kujali ''Minority societies za Viumbe kama hawa Bundi ambao ni wapweke sana Dunini'' kama walivyo hawa Bundi, na kuwa Dunia isiishie kwenye DEMOKRASIA za kupiga kura na Uchaguzi kwenye nchi zao peke yake.

    4.Kuwahakikishia watu na hasa huku Afrika ya kuwa Bundi sio ndege wa Uchuro ama kuashiria Misiba, na kama ingekuwa ni kweli mawazo hayo nadhani Bwana Kamanda ktk Ukoo wako hadi sasa ungebaki peke yako tu.

    5.Ni fundisho kumpa maisha ndege ama Kiumbe, tena aliyekuwa dis-advantaged (aliye dharauliwa na kutengwa na jamii) kama Bundi kuweza Kuishi nchini Ujerumani akila asali kwa maziwa Majuu!!!

    LA MWISHO NI KUWA UWASILIANE NA MALAKA ZAUJEREMENI IKIWEZEKANA KANSELA ANGEL MARKELEL HIYO ''Anannuki Empire'' IPATE IWAKILISHI KULE BUNGENI UJEREMENI BUNDESTAG PIA MAMLAKA YA ANANNUKI EMPIRE IPEWE RUHUSA KUWA NA BENDERA YAKE!

    ReplyDelete
  2. Ras Makunjas Reason nyingine Mbili kubwa sana za kuwafuga Bundi:

    6.Rangi yake Nyeusi ni moja ya Rangi za Bendera ya Ujerumani.

    7.Ktk Ngao ya Ujerumani (yaani kama ile Adam na Hawa yetu JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ile Ngao ya UJERUMANI INA NDEGE AITWAYE TAI KIINGEREZA NI EAGLE AU VULTURE AMBAYE NI JAMII YA BUNDI!

    ReplyDelete
  3. Kamanda Ras Makunja,mbona kuna baadhi ya wadaku wanasema kuwa Bundi wako wamekuwa wakiwatisha majirani zako walizunguka "Anunnaki Empire"

    ReplyDelete
  4. BabaMtukutu Kamanda Mkuu wa FFU Field marshal Ras Makunja,chonde chonde kamanda mbona midudu hiyo macho yanatisha unaipendea

    ReplyDelete
  5. Kamanda Ras Makunja inasemekana bundi wako wanakusaidia kufukuza msongomano wa wageni nyumbani kwako "Anunnaki Empire" a.k.a FFU Camp

    ReplyDelete
  6. Yule ndege aliye katika nembo ya ujerumani ni aina ya FONEX

    ReplyDelete
  7. baba mtukutu kamanda mkuu wa ffu field marshal Ras Makunja mtawala wa viumbe wa ajabu Anunnaki Alien,wenzio wanafuga chiriku,kasuku,ninga tetele sasa wewe na bundi wako ! nyuma yake kuna siri gani? mkuu! midege hiyo sio ya kuishi nayo katika makazi ya binadamu kamanda

    ReplyDelete
  8. mkuu wa kikosi kazi kamanda ras makunja kweli unatekeleza demokrasia ya ulaya kuwa kila kiumbe anastahili kuheshimiwa,wengine wanafuga mbwa wewe na bundi wako,tena unawatetea !
    Pia nakubaliana nawe bundi ni ndege wakimya sana

    ReplyDelete
  9. Ras Makunja hao bundi wako kaa nao huko huko, ukija vekesheni bongo hawakubaliki. kwanza sijui utafikia wapi maana jumba lako la kariakoo pale Aggrey na Kongo umeshapiga bei, sasa kuna mzinga wa golofa. Yaani hata ungefikia hapo mwenyekiti wa mtaa angekushtaki kwa FFU wenzio pale Msimbazi. Unasema bundi mkimya, kivipi. anavyowanga usiku huwa huwasikii. au wa huko ughaibuni hawawangi usiku

    -Mwana Aggrey

    ReplyDelete
  10. wewe ! Mwana wa Agrey,
    Madai yako ya kuwa hile nyumba ya kina kamanda imeuzwa si kweli kabisa,
    Nyumba hiliyopo kariakoo Mchikichi/Kongo Namba 18 ya ghorofa 5
    bado mali ya familia ya Kamanda wa FFU,Sema tu hii mududu Bundi anayo ifuga kwa kweli asije nayo kabisa Kariakoo,bundi wanatisha tena watatumalizia njiwa wetu.
    Mdau
    Jirani wa kamanda
    Mchikichi street,Kariakoo

    ReplyDelete
  11. Nyumba yao akina Ras makunja iliopo
    mchikichi St.18 hawajauza lile ghorofa wanalimiliki familia yake.
    Mdau
    Mtoto wa jiji
    Mtaa manyema

    ReplyDelete
  12. Anaefuga bundi ni mwanga mkubwa, lakini asiogopwe.

    ReplyDelete
  13. Kamanda Ras Makunja ni mwanamuziki wa aina yake,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...