Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.
Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond
Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Hongera sana Diamond. Binafsi nimeguswa na tendo ulilofanya. Mungu akuzidishie kila jema.

    ReplyDelete
  2. wangapi ni matajiri lkn si watoaji? Mungu akuzidishie Diamond.

    ReplyDelete
  3. Kila la Kheri kwa Kijana Naseeb Abdul kwa Ibada hii.

    Inshallah, Mwenyezi akuzidishie zaidi!

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Diamond!!! huu ni mfano wa Kuigwa...mimi nilikuwa sifuatilii muziki wa kizazi kipya kwa sababu ya umri wangu lakini kuanzia sasa nyimbo zako nitakuwa nazisikiliza

    ReplyDelete
  5. Mfano mzuri wa kuigwa alioonyesha kijana mdogo. Mungu akupe mara mia moja,kwa hakika hutapungukiwa pale ulipotoa bali utazidishiwa,poke baraka za Mungu.

    ReplyDelete
  6. Kijana wa "Kwetu Mbagala" umenigusa kwa kumkumbuka na kumuenzi Mzee mstaafu. Mungu hubariki sana mkono unaotoa na akujaze baraka tele kwa kipimo kilekile...Amen

    ReplyDelete
  7. You have touched heart too Diamond, last long as famous singer in Tanzania and beyond! Be blessed for that, it is a lesson to all of us on giving.

    ReplyDelete
  8. hongera umefanya vizuri lakini kwa usalama inabidi umwekee na dereva yeye mwenyewe hattoweza kuendesha sorry if I'm wrong

    ReplyDelete
  9. Mungu ainuliwe ktk kazi zako Diamond,umefanya kitu ambacho wengi wanapenda kufanyiwa na si kuwafanyia watu wengine,Ubarikiwe sana!

    ReplyDelete
  10. Diamond upo juuuuuuuuu!!!!!
    Upo juu sana mdogo wangu, kaza buti hivyo hivyo.
    Anzisha na Diamond Foundation watu wajaze mapesa ili uwasaidie wengi zaidi. Na kila show uwe unachangisha fedha kwa ajili ya watanzania wenye matatizo.
    Hongera sana. Sasa kila Msanii ajipime mwenyewe.

    ReplyDelete
  11. Mungu akubariki na kukuzishia kumbuka pia kusaidia masikini wa masikini zaidi nakushauri ukiweza fungua foundation maalum kwa ajili ya kusaidia watu masikini zaidi(The poorest of the poor)kwa sababu jina lako ni kubwa unaweza kutumia jina lako kukusanya donations kutoka vyanzo mbalimbali.Mkono unaotoa ndiyo mkono unaopokea Mungu akubariki na akulinde.

    ReplyDelete
  12. Hongera sana Diamond, Mungu akuzidishie pale ulipopunguza. Wasanii wengine siyo lazima na ninyi mtoe magari,saidieni wenye shida kwa chotote kidogo mlichonacho.

    ReplyDelete
  13. Mtoto wa mbagala nimekuzimia. Yule aliyekukataa achana nae. Mimi nimekukubali ubarikiwe maradufu

    ReplyDelete
  14. Sawa mdogo wangu, la kumbka dini yasema toa mono wa kulia usijue. So next time just do it kimya kimya!

    ReplyDelete
  15. Tabia ya wabongo kuiga iga utaona wasanii wengine nao wanaanza kutoa gari. Tafadhali buni kitu kingine cha kutoa si lazima ufanane na alichotoa Diamond. Hongera kijana kwa moyo uliouonyesha

    ReplyDelete
  16. Diamond umefanya kitu ambacho wengi tunashindwa kuthubutu!, hongera.

    ReplyDelete
  17. Da Diamond umempa Ngurumo pension ya aina yake! Safi sana. Hakika umefikiri na kutenda cha maana kama ni dereva wengine wajitolee!

    ReplyDelete
  18. Uungwana ni vitendo!

    Diamond umewabeba jamii ya Wasanii.

    Na ninyi Mashabiki mliocheza Muziki wa Mtu mzima miaka nenda miaka rudi tokea Uhuru kwa miaka zaidi ya 50 sasa, vipi?

    Kutoa kwenu kwa nyundo?

    ReplyDelete
  19. Je, mnamuacha vipi Mzee mzima Gurumo?

    Maafiasa wa Chama na Serikali nanyi mtakuwa mmesha Staafu mlishavuta chenu ama mnakaribia kustaafu kwa maana mtavuta chenu.

    Ni wazi ya kuwa ingawa hakuna Mkataba rasmi Bendi aliyo itumikia mkubwa tokea Uhuru miaka zaidi ya 50 ni ya Chama na Serikali na Taifa kwa ujumla, Mifiko ya Akiba ya uzeeni kama NSSF,LAPF, PSPF GEPF na NPF ni kipi mmemwandalia Mtumishi asiye Rasmi Gurumo angalau mtoe aibu zenu?

    Mmeshindwa hata zawadi za Kustaafu?

    ReplyDelete
  20. Mashabiki wa Muziki mamia kwa maelfu kwa mamilioni mpo wapiii ???

    Au umuhimu wa Nguli ulikuwa akiwa katika kuwatumkia kuwapa Burudani tu?, acheni hizo!

    ReplyDelete
  21. Mdau wa 19 ni kweli kabisa!

    Hiyo Mifuko uliyo itaja hapo ina Masifuri marefu san tu kwa wigni wa Mapesa, hivyo sioni ajabu kama watajikakamua wakatoa chohcote.

    La muhimu itakumbukwa ya kuwa Mzee Gurumo na Bendi yake amekuwa akitoa Burudani sana, sana, sana, katika Mikusanyiko hiyo hiyo ya Chama Kiserikali na Taifa kwa ujumla hata ktk Taasisi na Idara mbalimbali ikiwemo hiyo Mifuko kwenye Hafla zao Mzee mzima hakuwa nyuma.

    Nilisha wahi kuona mara kadhaa OTTU JAZZ BAND, MSONDO NGOMA akiwemo Mzee mzima Gurumo ikitoa burudani ktk Hafla zikifanyika kwenye Uwanja wa Mnazi Mmojo wa Arnautoglu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...