NYOTA ya mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata (pichani) amezidi kung’ara baada ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa upande kipato.
Kwa mujibu wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes kwa bara la Afrika (Forbes Africa) lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee aliyeingia katika orodha hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na kuzidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.
Katika orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiyo aliibuka namba moja na wengine sita pamoja na Flaviana wakibaki kutoa ushindani mkubwa kwa mlimbwende huyo wa Angola.
Mbali ya Flaviana, wanamitindo wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni Candice Swaenpoel, Katryn Kruger wote wakitokea Afrika Kusini, Ajak Deng, Grace Bol ( Sudan) na Liya Kebede wa Ethiopia.
Flaviana Matata aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania mwaka 2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora na baada ya kumaliza muda wake aliendelea na fani ya uanamitindo Afrika kusini na baadaye alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika makampuni makubwa ya uanamitindo ya Next Models International na sasa yuko Wilhelmina Models. A
kizungumza kutoka New York, Flaviana ameeleza kufurahia mafanikio haya hata hivyo ameongeza “Mpango wangu ni kuzidi kumweka Mungu mbele na kuhakikisha kuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu na kuiletea sifa familia yangu na nchi yangu”.
Hao Wanub wa South Sudna, vipi Mwanamitindo Alek wek aliyewahi kmtoa kamasi Naomi Campbell?
ReplyDeleteIlishatokea siku moja Jijini Paris -France kulikuwa na utambulisho wa Wanamitindo ikatokea Naomi akaenda hapo akitokea kwake London-UK alipofika aliuliza ALEK WEK amefikia Hoteli gani?,Wengi hawakujuwa umarufu wake lakini walipotafuta wakaona Hotel aliyofikia na hapo Naomi akaomba chumba Hotel iliyopo Opoosite.
Baada ya muda Naomi akiw Hotelieni kwake akampigia simu Alek Wek akiwa chumbani kwake na kumweleza ya kuwa anajua yeye Alek Wek Mpinzani wake kuwa ameshafika Paris!!!
anony 1-1 of 1
ReplyDeleteumeandika vitu gani mbona havieleweki
Anony wa Pili
ReplyDeleteHUELEWI KWA KUWA HUFAHAMU MAMDO YA DUNIA YANAVYOKWENDA.
Wabongo wengi hupenda kujifanya wajuaji kama wewe wakati wakiwa hawajui kitu. na NDIO MAANA HUNAUNALOLIJUA HAPO HIVYO ULITAKIWA USOME NA UWAACHIE WENYE KUYAJUA MAMBO.
MICHUZI KWA KUWA NI MWELEWA NDIO MAANA COMMENT AMEITUNDIKA
upo hapo?