Taswira za askari wa jadi wa jimbo la Tyrol huko Alpbach nchini Austia wakiingia kwa gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima ya Rais Jakaya Kikwete aliye katika mkutano wa Kamisheni ya Ulaya mjini humo. Historia ya askari hawa, wanaojulikana kama Schuetzenkompanie, inakwenda miaka ya 1810 wakati wa vita na watu wa Bavaria. Soma historia yao BOFYA HAPA
Sungusungu hao wakiendelea kuwasili
Kila mmoja ana gobole lililotengenezwa kienyeji
Watoto kwa wakubwa wamevutiwa na Sungusungu hao
Gwaride rasmi
Mdau anajiunga na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Austria Mhe Heinz Fischer (katikati), Rais wa Kamisheni ya Ulaya Mhe Jose Manuel Barroso (wa pili kushoto), Rais wa Mkutano wa Alpbach Dr Franz Fischer (kushoto) pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala
Duhhh Dunia kijiji!
ReplyDeleteIna maana Tanzania sisi kuwa na Sungusungu kuanzia huko Magu na Kwimba hadi Mijini kama Dar tuliona mbali mwanawane.
Yaani haya mambo huku Tanzania tunayadharau kumbe Majuu yapo?
Mugambo ni Sungusungu?
ReplyDeleteWajameeni kumbe na wazungu na wao washilumu
Duh!Kumbe sungu sungu wapo hadi Ulaya?
ReplyDeleteHuyu mdau kachomokea wapi peku? Duh haka kataajiriwa kabla ya kumaliza shule.
ReplyDeleteHahahahah!
ReplyDeleteWadau hapo juu,
Halafu wewe hapo Mtaani kwako ukipangiwa ulinde Sungu sungu usiku kucha na Mjumbe wa nyumab 10 unakuja juu na unakwepa zoezi hilo muhimu kwa usalama wako!!!
Si mchezo ndio maana Wasukuma na Wanyamwezi nchini Tanzania wanaitwa Wamarekani na Wazungu wa Kiafrika!
ReplyDeleteSi mmeona mambo yao ya Usungusungu hata Majuu yapo?