Ndugu wananchi;
Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kwa mara nyingine tena kutekeleza utaratibu wetu huu mzuri tuliojiwekea wa Rais kuzungumza na taifa kila  mwisho wa mwezi.
Ndugu Wananchi;

Mwezi Julai, 2013 ulikuwa wa neema kubwa ya wageni kwa nchi yetu wakiwemo watu na viongozi mashuhuri duniani. Natoa shukrani nyingi kwa Watanzania wenzangu kwa jinsi tulivyowapokea wageni wetu zaidi ya 1,700.  Wamefurahi kuwepo kwao nchini na wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu.  Wageni wetu wamekuwa wa manufaa makubwa kwa nchi yetu.  Wamesaidia kuitangaza Tanzania duniani na kuendeleza fursa za kukuza utalii, biashara na uwekezaji nchini na kwingineko katika Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. nimeipenda hotuba hii

    ReplyDelete
  2. jk ukiacha Obama anafuata niwewe!
    big up jk!!

    ReplyDelete
  3. Mheshimiwa Raisi na wananchi wa Tanzania napenda kutowa hongera sana kwa kuangaria mbali na siyo karibu au pa fupi maana ukisiliza hutuba hii inakuonyesha kwamba nani ni kiongozi na nani ametoka kwenye nchi ya watu wenye kuelewa maana ya maisha au ubinadamu ,Raisi Kikwete ametowa hutuba ya Uraisi na siyo hutuba ya kijinga kama iliyotolewa na Raisi kagame na baadhi ya watu wake alionao serikarini,wapende wasipende ukweli uko pale pale kama Raisi Museveni aliweza kuongea na baadhiya viongozi au makundi yaliyokuwa yanampinga je itakuwaje Raisi Kageme ashindwe kuelewa nini Raisi mwenziwe alicho kuwa akikisema, kwa kweli ushauri ulikuwa ni wa bure na pia kuna makundi ya watu wanaoipinga serikali yake ambao anaweza kuongea nao na pili congo ni ya wacongo si ya watusi au wahutu,Raisi nashukuru sana kwa hutuba yako nzuri sana imetupa nguvu na imeonyesha umekomaa kisiasa na uko na busara, waswahili usema damu ni nzito kuliko maji ,NINGEPENDA kumwambia kagame sisi hatuwezi kupiga kelele kama wewe sikiliza hutuba ya Raisi kikwete ukaa chini ufikirihe ungefanya nini wakati mwenzio alipokupa ushauri wa bure,serikari yako imetutukana sana sisi watanzania tunasema kama unataka amani tutaenda njia moja na ukifikiria Tanzania ni congo hiyo ni ndoto
    Hongera Raisi kwa kuwa kiongozi mwenye Busara na hekima na kuwa kiongozi shupavu sisi tuko nyuma yako na kama wanyarwnada wanataka kuleta mchezo wajaribu ndio watajuwa watoto wa mwalimu na wajukuu wa mwalimu si watu wa kuchezewa,mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Africa,
    yusef

    ReplyDelete
  4. Probably this is one of the best "wananchi speach" President JK
    had ever deliver to us, comparing to the past.

    His awareness of past and future development of our nation`s infurstructure & economy.

    Global leaders and friends
    recently visiting and invest in our country.

    The most interesting part of his speach last but at least is well caculeted diplomacy responce to our neighbouring countries
    avoiding further misundrstandings & retaliation of lowless & aimless words while we still need each other socialy & economicaly as East & Central Africa partners.

    Finaly with his kind words to us
    "wananchi" assurring us Tanzania is safe and still concetrating with it`s foreign policy.

    He ask each & every citizen play to Almighty-God to protect & bless Tanzania & Africa as a whole.

    Mickey "Mikidadi" Jones
    Denmark

    ReplyDelete
  5. Pamoja na wtnzania wengi, wenye uchu wa mali na madaraka, kumchukia Mhe Rais, lakini ukweli utabaki pale pale, huyu ni Raisi mwema mpaka sasa hivi hajawahi kutokea nchini mwetu, Ni mstaarabu sana, lugha za kistaarabu viongozi wengi duniani hawana, ukweli uko wazi Kagame ni mtu asiyeambilika, pia anahamu sana na tanzania, amewafanya raia wake, kuwa kama kuku kwa kumuogopa, sisi tutachapa wewe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...