Balozi wa Kenya nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Mutinda Mutiso akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nakala ya Kamusi ya Istilahi za Kidiplomasia(Diplomatic Terminologies Dictionary) wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza muda wake wa utumishi hapa nchini mwishoni mwa wiki.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.



KWA KAMUSI HIYO:
ReplyDeleteTumepigwa hapa Bao la KISIGINO NA WATANI ZETU WA JADI KENYA!
Enhee Watanzania ''WASWAHILI'' wenzangu kwa nini tokea jana hamjatuma Maoni hapa?...ni aibu ndio maana mpo kimya!
Eti oooh Kiswahili ndio lugha ya Taifa ya Tanzania wakati Kamusi imeandaliwa na Kenya?
Hivi wale Maprofesa kibao pale Chuo Kikuu UDSM Idara ya Kiswahili wanafanya Kazi gani?
Kwa nini hadi leo Tanzania na hasa hiyo UDSM ktk Idara ya Kiswahili haitoi Shahada ya Kwanza na Shahada ya Pili za Lugha ya Kiswahili?
Maprofesa Chuo Kikuu Darisalama fungeni mikanda kwa hii fedheha!!!