Picha na habari na Faustine Ruta
Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania ya Miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Peter Joseph Serukamba (Mbunge Kigoma Mjini) ilifanya ziara ya kukagua miundombinu ya bandari na viwanja vya ndege mkoani Kagera jana Agosti 14, 2013. 
Kamati hiyo mara baada ya kuwasili mkoani Kagera na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera ofisini kwake majira ya saa 5:00 asubuhi ilianza ziara yake mkoani hapa kwa kutembelea bandari za Bukoba na Kemondo kujionea miundombinu ya bandari hizo. 
Katika bandari ya Bukoba baada ya kutembelewa na kukaguliwa Kamati iliuagiza uongozi wa bandari kufanya ukarabati wa haraka katika sehemu ya abiria kwa kufumua paa ambao limezeeka na kullipandisha juu zaidi ili kuruhusu hewa zaidi katika eneo hilo na kweka paa jipya lisilovuja. 
Pia katika Bandari ya Kemondo Mwenyekiti wa kamati Mhe. Serukamba baada ya kusomewa taarifa alimwagiza Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi kuhakikisha mara moja nyumba za watumishi zilizoko katika eneo la bandari ya Kemondo zilizochukuliwa na Shirika la nyumba la Taifa zinarejeshwa kwa mmiliki wake wa awali ambaye ni bandari ya Kemondo. 
Katika hatua nyingine wajumbe wa Kamati walitembelea Wilayani Missenyi na kukagua eneo la Omukajunguti ambapo serikali inatarajia kujenga uwanja wa kimataifa wa ndege. 
Katika eneo hilo Kamati ilitoa maelekezo kwa taasisi inayohusika, Wizara na Halmashauri kukamilisha maandalizi ya kiwanja hicho. Kamati iliagiza Wizara ya Uchukuzi kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TIAA) pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kukaa pamoja na kuweka mipaka halisi ya kiwanja cha Omukajunguti pia kufanya tathimini na kuwalipa wananchi fidia zao ili kupisha ujenzi wa uwanja huo. 
Aidha katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba wajumbe wa Kamati waliridhika na maendeleo ya ujenzi na kumsisitiza Mkandarasi kuhakikisha anamaliza kazi zake kwa muda aliopewa kufikia Februari 2014. 
Aidha Wizara kuhakikisha inawalipa fidia wananchi ambao bado hawajalipwa fidia zao kiasi cha milioni 900 katika mwaka huu wa fedha 2013/2014.
Picha ya Pamoja Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe (mwenye suti) na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu  

Wajumbe wa Kamati Wakikagua Meli ya MV Victoria Katika Bandari ya Bukoba
Wajumbe wa Kamati Wakiwa Katika Eneo la Omukajunguti na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Wakipata Maelezo ya Eneo Hilo.
Uwanja wa Ndege Ukiwa Katika Matengenezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu Walifika kuukagua

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Safi sana. Nasubiri siku ije kila mkoa una airport angalau moja.
    @NduguAli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...