MAREHEMU MAMA FATUMA NINDI

Siku kama ya leo tarehe 12 augusti mwaka 2010 mama ulitutoka.Siku hii ilikuwa ngumu sana kwetu kwani si rahisi kuelezeka.

Mama kwetu ulikuwa si mama tu bali mshauri na rafiki yetu mkubwa.Huku mshauri na rafiki bora kwetu tu bali hata kwa marafiki na majirani zako ambao wote wanakukumbuka kila siku.

Kila nafsi itaonja mauti bali kwetu sisi wanao tunaona kama umetutoka mapema sana na katika muda ambao tulikuwa tunakuhitaji zaidi. Mama tulikupenda sana ila Mwenyezi Mungu alikupenda zaidi yetu na ndiyo maana akakutwaa.

Tutaendelea kutenda yale mema yote uliyotufundisha kubwa likiwa ni UPENDO.

Unakumbukwa na sisi wanao Anna,Patrick na James bila kusahau wajukuu zako Browne Kelvin(Costa) na Evelyn.

MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI MAMA,AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mungu ni sote, familia ya akina Fatuma, Anna, Patrick, James, Brown Kelvin na Evelyn inakuwaje?
    Mbele yake sote tutafika kwa vile ni wetu pamoja!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...