Mwenyekiti
wa Umoja wa Makatibu Mahsusi wa Wizara
ya Nishati na Madini (TAPSEA) Marcelina Mushumbusi (katikati) akizungumza na
watumishi wa Kada husika katika maadhimisho ya Siku ya Makatibu Mahsusi
Tanzania, Agosti 23, 2013. Maadhimisho hayo
yalifanyika Makao Makuu ya Wizara, Dar es Salaam.
Makatibu
Mahsusi wa Wizara ya Nishati na Madini wakijadili mafanikio na changamoto
ambazo wanazipata katika utendaji wao wa kazi, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya
Siku ya Makatibu Mahsusi Tanzania.
Makatibu
Mahsusi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja,
walipokutana kuadhimisha Siku ya Makatibu Mahsusi Tanzania.
Baadhi ya Makatibu
Mahsusi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja,
walipokutana kuadhimisha Siku ya Makatibu Mahsusi Tanzania.
Na George Mremi na
Hendrick Msangi
Mwenyekiti
wa Umoja wa Makatibu Mahsusi wa Wizara
ya Nishati na Madini (TAPSEA) Marcelina Mushumbusi amewataka watumishi wa Kada
hiyo katika Wizara husika kufanya kazi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa
mwajiri wao, Serikali na jamii nzima.
Akizungumza
katika Maadhimisho ya Siku ya Makatibu Mahsusi Tanzania yaliyofanyika Makao
Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam, Mushumbusi aliwasisitiza Makatibu Mahsusi
hao kutoa huduma kwa weledi na kuwataka kuwa na upendo, umoja, na kusaidiana
ili kufanikisha majukumu yao ya kila siku.
Wakiadhimisha
siku hiyo muhimu, Makatibu Mahsusi wa Wizara ya Nishati na Madini walikutana
pamoja kujadili mafanikio na changamoto ambazo wanazipata katika utendaji wao
wa kazi.
Mushumbusi
alitumia fursa hiyo kuomba Uongozi wa Wizara kutoa mafunzo ya weledi na maadili
bora ya kazi kwa watumishi wa Kada hiyo.
Aidha,
alishauri watumishi wengine wote wa Wizara wapewe mafunzo ya aina hiyo kulingana
na taaluma zao ili kuboresha utendaji wa kazi za serikali kwa manufaa ya
Watanzania wote.
Mwenyekiti
huyo alimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi kwa kutoa fursa ya wao
kujiendeleza kielimu hali ambayo
inawasaidia kuwa na ufanisi katika utendaji wao wa kazi.
Aliwataka
Makatibu Mahsusi kuchangamkia fursa hiyo ya elimu kwa kuongeza ujuzi katika
fani yao na pia aliwapa changamoto kusoma fani nyingine ambazo zitawasaidia
kuendana na mabadiliko yanayotokana na kukua kwa teknolojia duniani kote.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...