Mama Tunu Pinda
MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda amesema kuna haja ya kuweka juhudi za makusudi za kuwawezesha wasichana wote nchini kuondokana na aibu zinazowazuia kuhudhuria masomo yao kila siku.

Amesema kukosekana kwa vifaa vya kujisetiri miongoni mwa wasichana waliofikia balehe, ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wakose masomo kati ya siku 30 hadi 70 kwa mwaka jambo ambalo linachangia kudorora kwa elimu miongoni mwao.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Agosti 20, 2013) wakati akizindua Mradi wa Hakuna Wasichoweza katika Shule ya Msingi Chilongola, iliyoko Manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani Mtwara. Mradi huo unafadhiliwa na Taasisi ya T-MARC inayojihusisha na Masuala ya Afya na Maendeleo, umelenga kuwafikia wasichana 10,000 katika wilaya mbili za mkoa wa Mtwara, yaani Manispaa ya Mtwara Mikindani na Wilaya ya Mtwara Vijijini.

“Wasichana wengi wanapopata siku zao, hushindwa kuhudhuria masomo yao kati ya siku tatu hadi saba kwa mwezi au siku kati ya siku 30 hadi 70 kwa mwaka. Hii husababishwa na wasichana hawa kukosa nyenzo za uhakika za kujisitiri wakiwa shuleni. Wengi wao huamua kubaki nyumbani hadi pale mizinguko yao itakapokwisha ili kuepuka kuaibika...,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mwanamke wa kiafrika no mkorogo keep it up mum

    ReplyDelete
  2. labda kuna sababu zingine,hiyo si sababu,tumetoka huko enzi zile na shule tulienda kabla hata havijaja vifaa vya kisasa.Kwanza tuongelee ubora wa hiyo elimu mnayosema wasichana wapate.Hakika kuacha kwenda shule kwa suala hilo ni utoro na si kitu kingine.

    ReplyDelete
  3. Mimi huyu mama huwa namfagilia wawaaaaaaaaaaaaa! Natural beauty

    ReplyDelete
  4. Sawasawa.

    Mama Mkulima, Mama Pinda.

    Natural African, More African, TRULLY African!

    ReplyDelete
  5. Miss Tanzania:

    Ili kuwapa Mwamko Wasichana ktk suala la Urembo hasa wa asilia ili waache kuvaa manyoya ya farasi vichwani na matumizi ya mikorogo kama vigezo vya kusaka Urembo na Ulimbwende mngekuwa mnawaita akina mama kama huyu Mama Pinda, angalau Wasichana wanaweza kujiamini na wakajifunza ya kuwa BEAUTIFUL IS NATURALLY GOD GIVEN AND SMARTNESS IS AN ART !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...