Waziri wa Nchi Ofisi ya Mamaku wa Rais Mazingira,Dkt. Terezya Huvisa akizungumza na waandishi wa habari ofisin kwake jijini dar es salaam leo kuhusu tamko la serikali la upigaji marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchi.(Picha na Ofisi ya Makamu ya wa Rais.)
Na Ofisi ya Makamu wa Rais
Serikali imepiga marufuku ungizaji, utengenezaji, uuzaji, na utumiaji wa mifuko ya plastiki. hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais(mazingira) Dk Terezya Huvisa alipokuwa akizungumza na waandishi ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Dkt. Hufisa ameeleza kuwa Serikali imehamua kuchukua hatua hii ili kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la kusambaa na kutapakaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo baada ya matumizi yake huishia kwenye uchafuzi wa mazingira .
Alisisitiza kuwa, Zuio hili linahusu mifuko yote ya Plastiki ya kubebea bidhaa toka madukani, sokoni na majumbani isipokuwa mifuko yenye unene wa maikroni mia moja inayooza (bio-digradable) na vifungashio vya bidhaa mbali mbali kama vile vifaa vya mahospitalini.
“Marufuku hii inapaswa kuzingatiwa na wenye viwanda, wenye maduka na wananchi kwa ujumla ili kutokomeza kuenea kwa taka zinazotokana na mifuko ya plastiki kwenye mazingira.” Alisema.
Dkt Hufisa aliendela kusema kuwa, Jitihada zinatakiwa zifanywe ili kuhakikisha kuwa marufuku hii inazingatiwa, na misako ya watu wanaofanya biashara ya mifuko hii ifanyike katika maeneo yote ndani ya nchi yetu, na watakaokiuka wachukuliwe hatua, ikiwa ni pamoja na kufanikishwa katika vyombo vya sheria .
Imeelezwa kuwa madhara yanayosababishwa na mifuko ya plastiki ni pamoja na uharibifu wa udongo unaotokana na kuunguzwa kwa plastiki hizi na hivyo kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama ,kutooza kiurahisi wa njia za kiasili (non-biodegradable) kuzagaa katika mito, maziwa, bahari na nchi kavu hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai wanaoishi katika mazingira.
wenzenu Zanzibar walishaliona hilo kitambo....hv mlikua wapi?
ReplyDeletebest news in a looong time. maana ilishakuwa mifuko janga la taifa. pongezi kwa kufanya jambo la msingi
ReplyDeleteMsi ishie tu kutangaza sheria bali kuhisimamia na kuhakikisha inatekelezwa
ReplyDeleteMimi nawapongeza kwa hilo tamko. Mifuko ya plastiki ni kero hasa kwa mazingira na nilikuwa nashangaa kwanini serikali na wizara usika wamekaa kimya sana.
ReplyDeleteNaomba hilo tamko livanye kazi sio maneno tu.
Mimi nakumbuka ilikwisha pigwa marufuku lakini wakaingiza " isipokuwa mifuko yenye unene Fulani" hapo ndipo tatizo linapoanzia kwa sababu huo unene ndio unaochakachuliwa na kubaki hadithi za alfu lela ulela! The best thing is a unirvesal ban of use of any plastic bag" hapo ndipo tutafanikiwa lakini ukiweka isipokuwa hilo tayari ni tatizo kwa kuwa hiyo inawapa watu mwanya wa kudanganya na watu wengine kutengeneza mwanya wa rushwa na tatizo litabaki pale pale.
ReplyDeleteKwa hiyo basi pamoja na kuunga mkono tamko ni vizuri tuzuie mifuko ya aina zote siyo baadhi.
Hongera kwa hilo Dkt. LAKINI Dkt,lingine kubwa zaidi ambalo linatisha ni VYOMBO VYA PLASTIKI, mbona navyo havina VIWANGO PIA si HATARI kwa afya ya binadamu?!!! Hii ikiwa ni pamoja na matumizi ya chupa za plastiki zaidi ya mara moja. Kwingineko duniani wanapiga marufuku matumizi zaidi ya mara moja, kwa mfano kutumizi chupa ileile ya plastiki uliyonunulia maji au soda kwa matumizi ya majumbani n.k. Je, hivi havina hatari pia kwa Tanzania?
ReplyDeleteMsalieni Mtume jamani kwani mfuko wa rambo una kazi kibao. Nazo ni kama ifuatavyo:
ReplyDelete1.Suti kesi kwa ajili ya safari.
2.Choo kikubwa kwa kujistiri.
3.lunchi boksi kubebea chakula.
4.Shopping begi
5.sefu kwa kuhifadhi mihela
6.bango la matangazo kibiashara
7.brifu kesi
8.skuli begi
9.jarida/faili buku la kesi polisi
Wajameni tueshimu mifuko ya rambo kwani tumetoka nayo mbali na manufaa yake ni kedekede.
Kutamka ni jambo moja,na utekelezaji ni jambo jingine,let us wait and see.
ReplyDeleteHakuna jipya ni marudio tu ya marufuku ya miaka michache iliyopita.Usimamizi ni sifuri.
ReplyDeletembona kama kuna waakti walitangaza hivyi hivyo muda ila waziri hakuwa huyu. Hakuna hatua zilizochukuliwa mpaka leo, wanatangaza tena ni vizuri. Sheria ya NEMC 2994 ya mazingiria iko wapi? Sheria na Public health 2009 iko wapi? mbona hamzitumii na kuwaadhibu wanaokosea na sio kwenye plastic tu. Jitahidini kidogo kidogo wizara ya afya na makamu wa rais mazingira mtafika tu. Ila tuna matatizo mengi sana ya kiafya yatokanayo na mazingira hapa nchini Tz. Mungu anatupenda sana kwa kutuepusha na magonjwa. Mfano ukichoma moto plastic hiyo hewa yake ao moshi wake ni highly carcinogenic, na iansambaa hewani sio kwa mchomaji tu mana hewa ahina limit jamani, sasa hivyo vinavyotokana na plastic kuchomwa vina uwezo wa kukaa hewani au kwenye mazingira kwa muda mrefu na halafu vinasababisha cancer. Ndio mana nasema Mungu anatupenda sana watanzania na kutuepushia magonjwa hayo. Nje wanakuwa na sehemu special za kutupia takataka kwa kutokana na aina na wao hawendi kuchoma moto la hasha! Wanafanya recycling! Hata ukikata mti hutupi tu unakuchukuliwa na wabeba taka kwenye special areas za kuutupa. Taratibu waziri tutafika tu.
ReplyDeletewhat about those who have employed themselves by selling plastic bags? what about the industries that make plastic bags? and what will be the replacement of the plastics bags?
ReplyDeleteHas the government done enough research about the other side effect of abandoning the plastic bags?
i would like the government to provide the impacts of plastic bags expertly to the society and how the society will benefit from the new law
Anoni mmoja hapo juu ametoa angalizo zuri sana juu ya faida ya hiyo mifuko.Tatizo wengi wetu hatuliangalii jambo kwa upande wa pili! Mimi nasapoti hiyo mifuko ina faida sana kuliko hasara zake! Je kuna mbadala wa uhakika? Huyo waziri kafanya utafiti nchi ngapi zinazofanana na Tanzania zimepiga marufuku? sio kuiga Marekani.Muhimu ni jinsi unavyo handle waste materials zako baada ya matumizi!!Mbona Sigara zina madhara lakini kiwanda cha TCC hatujakifunga hatujaifunga?Usikute wengine mnaotoa hayo mawazo mmesomea kantalamba ka mie,darasa la 1 mpaka la 7 madaftali kwenye fuko la rambo.
ReplyDeleteKusema na kutenda ni tofauti. Nakubaliana na wanakumbusha kwamba jambo hili ni marudio 100% mpaka hicho kipengele cha isipokuwa unene flan ambacho kwa hakuna msimamiaji wa sheria balia mtangazaji mambo yanaendelea vilevile.
ReplyDeleteWhat's the alternative? Elimu haijatolewa ipasavyo watu watumie nini mbadala ya mifuko hii. Ingawa leo ni mapema sana kutekeleza hii, nimepita mitaa ya kati na kununua chapati za brekfast.....nikafungiwa kwenye foil na kupewa mfuko wa plastiki!
ReplyDeleteTUNAMWOMBA MH WAZIRI ALIYETOA TAMKO HILO NA ASEME AMEANDAA NINI KITUMIKE BADALA YA MIFUKO YA PLASTIC. VINGINEVO NITASEMA KUSEMA NI RAHISI ILI KUJITAFUTIA UMAARUFU FULANI LAKINI UTEKELEZAJI WAKE KIMATENDO UKO WAPI? UWEKWE WAZI PIA ILI TUJUE KUWA MH YUKO SERIOUS NA SWALA ZIMA
ReplyDeleteTatizo siyo plastic bags ni kufeli kuikusanya na recycle - uchafu wa manispaa tu. mbona uingeteza america sio makufuru?
ReplyDelete