
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Mh. Jerry Silaa akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chimbo
School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa redio Clouds na TV
Harris Kapiga wakati alipofika kwenye chimbo hilo kuzungumza na vijana
baada ya kuitikia mwaliko kutoka kwa Mwenyekiti
huyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Mh. Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa
Mwenyekiti wa Chimbo School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa
redio Clouds na TV Harris Kapiga.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Mh. Jerry Silaa akitema cheche kwa vijana na kuwatia
moyo.
Mmoja wa vijana akimuuliza maswali Mstahiki Meya
Jerry Silaa.
Na.Mwandishi wetu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Mh. Jerry Silaa akiwa katika ya nchi ya Ahadi Sinza Kamanyola
amefunguka kuhusiana na namna gani kijana anaweza kuishi ndoto
zake.
Moja ya mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na kijana
kujitambua na kujua nini hasa anataka na anapata vipi kwa maandalizi
ya kutimiza nia yake.
Mh. Jerry pia amechambua mada hiyo kwa marefu na
vijana kuonekana kumuelewa ipasavyo na hivyo kubaki kazi kwao
kutekeleza na kuyafanyia kazi yale aliyoyazungumza, ikiwemo kujua
lengo lao hasa ni nini na kujipima wanautayari wa kiasi gani katika
kutekeleza hilo lengo na kubwa zaidi ni uthubutu wa kufanya jambo
lenyewe.
Katika mazungumzo yake kilichowavutia vijana wengi
zaidi ni pale alipowaeleza kuwa yeye Mstahiki alithubutu kugombea
udiwani ndani ya kata ya Ukonga akiwa na umri wa miaka 23 na
kufanikiwa kushinda.
Ni jambo la kujivujia kuwa na vijana hasa kama
mstahiki Jerry Silaa ambaye pamoja na kuwa Mstahiki Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu na
Kamati Kuu ya Chama tawala cha CCM Taifa.
Pamoja na hayo Mh. Jerry Silaa amewaeleza vijana
kutambua hizo ndoto ni za nani hasa na ni nani wakuzifanikisha kama si
wenyewe.
Aidha, zaidi ya hapo amewaasa vijana kuwa na majibu
ama matokeo ya kila wanalofanyia kazi "being result oriented" na
kupata kile wanachokitaka kwa kuzingatia lengo pamoja na muda
kiutendaji.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Mh. Jerry Silaa katika picha ya pamoja na vijana waliojitokeza
kumsikiliza wakati akifunguka kuhusuiana na namna gani kijana anaweza
kuishi ndoto yake.
Blog ya Jamii:Naomba niende nje ya Mada Kidogo.HALMASHAURI YA WILAYA YA TEMEKE-Kuna hii barabara ya Kilwa.Kutoka pale round about sijui ndiyo bandari/kurasini kuelekea Mivinjeni,Ufundi,nk.Kuna kipindi fulani MKUU wa nchi alipanda miti pale.Miti ikamwagiliziwa wiki ya 1,2,3....kilichotokea baadae.....Ninavyotoka mara 1-1 kwenda huko "DUNIANI" sehemu kama zile 'WENZETU'wanajenga Seng'eng'e ili raia wasitakize na kuharibu vegetation(Ni kuvuka kwenye Zebra tu),na kuna watu wanalipwa kwa kumwagilia maji maua,miti nk..Yaani barabara zao zinapendeza kweli kweli.You cannot teach an old dog new tricks lakini..........
ReplyDeleteDavid V
mjomba hicho kiti ulichokalia muheshimiwa uliyetembelewa na meya sio kiti cha shughuli za kiofisi ! hicho ni kiti cha meza ya kulia chakula majumbani..kitakupa matatizo ya mgongo sanaaa...tuache longo longo bongo....ofisini ni nzuri ila hicho kiti kinatoa dosari sana..vipi haukukujua ni kiti gani kinatumika ktk shughuli za kiofisi ? anayway, ujumbe wa huyo meya naukubali kabisa !! na hizo nondo dirishani mh !! sijuwi pakishika moto hapo utatoka vipi humo ndani !! I am just saying....
ReplyDeleteWewe unayesema habari za nondo, unaishi wapi?na hata kama upo ughaibuni na umegoma kujenga kwenu, yakupasa ujue ujengaji wa ughaibuni na Bongoland ni vitu vi2 tofauti.
ReplyDeleteBila Nondo,unawaalika "Wajasiriamali" wa usiku na kufanya kazi yao iwe nyepesi.
Ni kweli uwekaji wa nondo hivyo ni hatari pakitokea dharura ila "Ndipo kama nchi tulikofikia"