Picha na Habari na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya BILELE FC imelazimika kupigana kufa na kupona ili waweze kutinga hatua ya fainali katika michuano ya Kombe la Kagasheki ikicheza dakika 90 na timu ya Kitendaguro fc bila ya kufungana. Baada ya kuongezwa 30 Bilele FC imeweza kuifunga timu hiyo maarufu kwa jina la Makhirikhiri yeye maskani yake Kitendaguro - Kibeta.
Bao la pekee la timu ya Bilele limefungwa dakika kipindi cha kwanza cha dakika 120 na mchezaji Ndomondo, huku wakicheza pungufu baada ya mwenzao kupewa kadi nyekundu katika kipindi cha pili cha dakika 90.
Ushindi huu unawasogeza Bilele hatua ya Fainali wakimsubiri mshindi wa kesho kati ya timu ya Kashai Fc na timu Rwamishenye Fc mtanange utakaochezwa kesho Jumatano saa 10.00 jioni hapo hapo uwanja wa Kaitaba.


Huu ndio uwanja unaotumika kwa premier league? Kama ndio huu malalamiko ya timu kuhusu kaitaba ni ya kufanyia kazi haraka. Unawezaje kuweka mpira chini ktk hali kama hiyo!!
ReplyDelete