Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na walimu wa kike wa Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 02 Agosti 2013 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Lengo la mkutano huo likiwa kujadili kero mbalimbali za walimu pamoja na kuzitaftia ufumbuzi. Pamoja na kero mbalimbali zilizowasilishwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa maelekezo kwa Halmsahauri ya Manispaa kushughulikia kero zinazowezekana ikiwepo madai ya likizo na mengineyo. Kwa yale yaliyo nje ya uwezo wa Manispaa aliahidi kuyachukua na kuyafikisha panapohusika ili yaweze kutaftiwa ufumbuzi. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Kushoto ni Afsa Elimu Taaluma Mkoa wa Rukwa Bi Catherine Mashalla.
Katika kikao hicho walimu walitoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kufuta chama cha waalim (CWT) kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiwakata waalim mishahara kwa mda mrefu bila kuwa na msaada wowote kwao pindi wanapouhitaji. Mapendekezo mengine ni kupunguza idadi ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka tisa hivi sasa na kuwawekea masomo yatakayowawezesha kusoma na kuandika kuliko hivi sasa ambapo masomo ni mengi na huwachanganya watoto. Hata hivo Mkuu wa Mkoa aliweka bayana kuwa ni vyema chama hicho kikaona ni jinsi gani ya kuwanufaisha zaidi walimu kwa kujiwekea utaratibu wa kuwakopesha au kuwasaidia kwa njia nyingine kiuchumi.
Sehemu ya waalimu waliohudhuria katika Mkutano huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwashauri waalim kutokopa katika taasisi zisizo rasmi ambazo riba zake ni kubwa kupita kiasi. Alisema taasisi nyingi za namna hiyo zimechangia kufanya maisha ya walimu wengi kuwa magumu na badala ya kuwa msaada kwao inageuka na kuwa kero.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Bi Witness Maeda akitoa kero mbalimbali wanazokabiliana nazo waalim ikiwepo uhaba madarasa, mabweni, bwalo na maabara chuoni hapo. Kwa ujumla kero zilizowasilishwa ziligusia mishahara hafifu ya walimu, uhaba na ubovu wa vyumba vya madarasa, kucheleweshewa madai yao ya mishahara na nauli (Salary Arears), kupandiswa madaraja na uhaba wa mafunzo ya mara kwa mara kuweza kukabiliana ni mabadiliko ya mitaala mipya.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa www.rukwareview.blogspot.com)
Nafikiri kero za walimu wa kike hazina tofaiti kubwa na za wenzao wa kiume. Kuliko kuzibagua, ingekuwa rahisi kwake kuzishughulikia zote pamoja. Hii ingeokoa muda wake pia.
ReplyDeleteUkumbi mzuri.
ReplyDeleteHilo la chama cha walimu, limelalamikiwa muda mrefu kwani wanaofaidika ni viongozi tu.
Walimu wanaishia makato ya kila mwezi.
Kama kawaida "Bongo tambarare"
Hongera sana wa andaaji wa majadiliano haya. Hongera Eng. Hon.Manyanya kwa kuwa mstari wa mbele kupigania haki za kina mama. Matatizo yetu ni mara dufu ya yale ya kina baba. tuna kila sababu ya kukutana na kujadili na kusikilizwa kama wanawake pekee.
ReplyDeleteEng. Manyanya is simply the best of all regional commissioners! Hongera sana mama. Mwenyezi Mungu azidi kukubariki kwa kujali shida za wananchi wa mkoa wako. Laiti kama RCs wote wangefanya nusu tu ya juhudi zako, nchi hii ingekuwa mbali sana. Na hicho chama cha waalimu (CWT) kinafanya "day-light" robery kwa waalimu wa Tanzania. Wamekatwa mishahara yao kwa muda mrefu kwa ajili ya kujenga jengo la waalimu pale Ilala Dar (Mwalimu House) ambalo lilishakamilika tangu 2009 na linazalisha pesa kibao lakini hadi sasa waalimu bado wanakatwa mishahara. Huu ni wizi wa mchana kweupe na kwa kweli Serikali ni lazima iingilie kati ufisadi huo usio na kificho wala aibu. Mwalimu House hutoza kodi ya zaidi ya Sh. 120 milioni kwa mwaka kwa orofa (floor) moja tu. ni jengo la orofa nane. Angalia ni kiasi gani cha pesa kinazalishwa lakini ni mara ngapi waalimu wamepewa gawio kutokana na kitegauchumi hicho????? CWT ache ni wizi. Na Serikali fungueni macho. Mkiwasaidia walimu mtapata thawabu nyingi sana licha ya kuwa ni wajibu wenu.
ReplyDeleteMdau wa kwanza ameliweka sawa,kwamba kero hazikuwa maalum kwa walimu wa kike hivyo mkuu hakuwa na sababu ya kutenganisha.Ingekuwa ni matatizo ya kipekee kwa walimu wa kike hapo sawa,lakini hii inapunguza mshikamano kati yao ambapo walimu wa kike wanaona wamepewa uzito na wa kiume wameachwa: divide and rule
ReplyDelete