Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally Nasoro Rufunga ametoa wito kwa wamiliki wa mashine za kuchambua pamba,kuanza kutengeneza nyuzi ili kuongeza thamani ya zao la Pamba katika kukabiliana na bei ya soko la dunia.
Mheshimiwa Rufunga ametoa wito huo mwisho wa wiki alipotembelea kiwanda cha Afrisian kilichopo mjini Shinyanga, katika ziara yake ya kawaida ya kuona shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi.
Amewashauri wamiliki wa mashine za kuchambua pamba kuboresha pamba hiyo ili kuzuia wawekezaji wa Kichina wanaojenga viwanda vya nguo hapa Shinyanga wasichambue pamba, badala yake wabaki na viwanda vya nguo na wanunue malighafi za nyuzi kutoka kwenye viwanda vya ndani ili kutodhoofisha viwanda vya Wazawa.
Aidha, aliwahimiza wamiliki wa mashine za kuchambua pamba wajitangaze ili wananchi na wadau wafahamu shughuli wanazofanya,kwani wana mchango mkubwa kwenye pato la Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Awali, Mkurugenzi wa Afrisian alimweleza Mkuu wa Mkoa changamoto zinazowakabili wenye mashine za kuchambua pamba kuwa ni bei ya pamba kushuka, na kutokuwa na mbinu bora za kisasa za kilimo hivyo kuzalisha pamba kidogo sana tofauti na nchi zingine.
Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Shinyanga


.jpg)
Ni Ushauri mzuri toka kwa RC Lufunga.Kama alivyogusia mmiliki wa Afrisian kuna changamoto kuu mbili
ReplyDelete1.Kushuka kwa Bei ya Pamba na hasa Pamba Mbegu toka kwa wakulima.Hii inafanya Wakulima kutovutiwa na kilimo cha Pamba ukilinganisha na gharama kubwa za uzalishaji na hivyo kuhamia kwenye mazao mengine yenye Tija kama Alizeti,Choroko n.k
2.Ubora wa Pamba Mbegu na hata Pamba Nyuzi ambazo hatimae husokotwa Nyuzi.Ili kupata nyuzi bora ni lazima Pamba Mbegu na Pamba Nyuzi ziwe na viwango vyenye ubora wa hali ya juu ili kuzalisha bidhaa bora zenye ushindani kwenye masoko mbalimbali Duniani.Changamoto kubwa ni usafi na ubora wa Pamba yetu ukilinganisha na Pamba inayozalishwa na nchi shindani.
Hapa ndipo wadau wote wa Sekta ndogo ya Pamba (Wakulima,Ginners,Mabenki,Serikali/Maofisa ugani na wanasiasa) wanatakiwa kutilia mkazo Ili kupunguza tatizo la Usafi wa Pamba (Contamination).
Ieleweke kuwa Wakulima kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuumizwa na mizani za wanunuzi hivyo nao kujibu mapigo kwa kutozingatia kanuni bora za usafi wa Pamba jamboree ambalo linaifanya Pamba yetu kutopata Bei nzuri (Premium) na badala yake kupata Bei ya chini (Discounted) jambo ambalo lisipotiliwa mkazo zao la Pamba litabaki historia.