Shirika la Afya Muhimbili liliingia mkataba wa pango na REGENT STORE mnamo mwaka 1987 ambapo katika mkataba huo makubaliano yalikuwa kwa REGENT STORE kujenga jengo ili litumike kuendesha biashara ya SUPERMARKET katika eneo la Hospitali kwa ajili ya mahitaji ya wagonjwa pamoja na wafanyakazi.
Mkataba huo ulikuwa wa miaka mitano yaani kuanzia mwaka 1987 hadi mwaka 1992 ambapo REGENT STORE alitakiwa kuwa ameishajenga jengo husika pamoja na kuendesha biashara ya SUPERMARKET katika hilo jengo kwa kipindi cha miaka mitano na kukabidhi jengo kwa Hospitali.
Kilichotokea:

Hata hivyo, baada ya miaka hiyo mitano kuisha, REGENT STORE hakukabidhi jengo hilo kwa Hospitali kwa mujibu wa mkataba kwa madai kuwa alikuwa hajarudisha gharama zake za ujenzi. Kutokana na madai hayo kuwa alikuwa hajarudisha gharama zake za ujenzi, Hospitali ilikubali kumwongezea muda wa miaka mitatu kuanzia 1992 hadi 1995.

Pamoja na Hospitali kumwongenzea miaka mitatu, ilipoisha miaka hiyo mitatu, REGENT STORE hakuonesha nia ya kukabidhi jengo kwa Hospitali, na badala yake aliendelea kulitumia bila ya mkataba wa aina yoyote na bila kukubali kukaa mezani kuzungumza na kutatua suala hilo. REGENT STORE aliamua kuendelea kutumia jengo hilo kinyume na taratibu na sheria za nchi kwa kuwa mkataba ulikuwa umeisha na nyongeza ya muda aliopewa pia ilikuwa imeisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Sasa hapo kulikuwa na Supermarket?
    ama "Magenge"?

    Vipi na ile Benki yetu ya wazawa NMB nayo imebomolewa?

    Kwa jinsi Muhimbili ilivyo ni Medical City kwa hadhi hiyo, panatakiwa pawe na SUPERMARKET ya ukweli ni aibu mfanyakazi anatoka kazini ana anza kutafuta wapi akanunue mahitaji muhimu.
    Hospitali zenye hadhi ya Muhimbili huko duniani, ukiwa ndani ya Hospitali unapata mahitaji yote ndani.

    Swali ni je SUPERMARKET itajengwa ama sasa ni mwendo mdundo hadi maeneo ya "Fire" ili upate maji?

    ReplyDelete
  2. KUNA UBAYA GANI KWANI HATA WAWEKEZAJI WA NJE WAJAO HUKO SI NAO WANAFANYA HIVYOHIVYO?AU KWAKUA HUYO NI MKONONGO MWENZENU?KUNA WAKATI KULE KTK MADINI SI ILIKUA HIVIHIVI KWAMBA WANAPATA HASARA HIVYO WAPUNGUZIWE KODI, KUNA WENGINE WAKAOMBA MICHANGA IKAPEMBULIWE KWAO NJE TUKAKUBALI PIA,MIE NAONA NI KAWAIDA TU NA HAKUNA UBAYA WOWOTE.

    ReplyDelete
  3. Bora yamevunjwa hayaendani na hadhi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili!!!

    Panatakiwa Muwekezaji mwenye Viwango vya juu na uwezo mkubwa wa Kifedha kujenga majengo yenye hadhi zaidi.

    ReplyDelete
  4. REGENT STORE ipo wapi hapo?

    ndio hayo Mabanda kama ya Gongo Keko?

    Mjomba Michuzi tafadhali wasaidie hao Muhimbili maana TAARIFA HII NA PICHA HIZI VIKIFIKA UBALOZI WA UINGEREZA HAPA TANZANIA WENYEWE WAKISIKIA HUKO UK JINSI HADHI YAO ILIVYOSHUSHWA WATAKUJA KUDAI FIDIA KUBWA SANA!!!

    Toka lini REGENT ikawa Mabanda ya papa?

    Mnacheza nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...