Kata ya Iwawa ilipo shule hiyo.
 
Na Edwin Moshi wa
Globu ya Jamii, Makete
Wafunzi wa shule ya sekondari Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe wamekiri uwepo wa wanafunzi wenzao ambao wanajihusisha na vitendo vya ngono na wengine wanaishi na virusi vya UKIMWI, licha ya jamii kudhani kuwa wanafunzi hawawezi kuwa na virusi hivyo kwa minajili kwamba bado ni wadogo.
Hayo yamebainika baada ya mtandao huu kufanya mahojiano ya kina na baadhi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hivi karibuni kwa ruhusa ya mkuu wa shule hiyo Bw. Christopher Haule hapo kufuatia wananchi wengi wilayani hapo kudhani kuwa wanafunzi hao hawana maambukizi ya VVU  kwa kuwa ni wadogo na huwenda hawajaanza kujihusisha na vitendo vya ngono.
Mwanafunzi mmoja (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) amesema ana marafiki zake zaidi ya watano ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI na hajui walivipataje, hivyo anaamini wapo wanafunzi wengi ambao wana maambukizi. kusoma taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Makosa NYETI kama haya yanatakiwa adhabu kali itolewe:

    1.Ubakaji,
    2.Ufisadi,
    3.Uhujumu nchi,
    4.Rushwa,
    5.Wizi.

    Dunia imepiga marufuku Adhabu ya Kifo lakini kwa haya Matano (5) Makosa hapo juu ipo kila sababu kutolewa kwa adhabu kali sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...