Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu na kulia kwa Mengi ni Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha NBC jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kushoto) akiwatambulisha baadhi ya maofisa katika kitengo hicho katika hafla hiyo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akifurahi na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa na Uwekezaji, Andre Potgieter katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akishikana mikono na Meneja Uhusiano wa NBC, Makyalen Marealle katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya uzinduzi wa kitengo hicho. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.
Naam mme mwita Mzee Mengi mbona Bilionea YM wa Yanga naye hamkumuita?
ReplyDeletewanaitwa wale wanaopata fedha kihalali
ReplyDeleteHahahahaha !!!,
ReplyDeleteNiacheni nicheke!
Mdau wa Pili ama kweli kutika kwa debe ndani mshindo mtupu, katika haya maisha yetu pana watu wanatisha kwa muonekano na majigambo!
Lakini ukweli wa mambo wanaujua Watumishi wetu wanaotuwekea Mapesa yetu kwa idadi na vyanzo, ndio pale unakuta Maulidi yana fanyika Mashekhe wa kuhudhuria wanachaguliwa!, yaani hata safu ya Madrassa ama Waandazi wa ubwabwa pia wa Maulidi imekosekana nafasi?,,,mpo hapo?