Ndege Ndogo ya Shirika binafsi la Ndege la TANZANAIR iliyokuwa ikitokea Mjini Bukoba kuelekea Jijini Dar es Salaam kupitia Zanzibar, imelazimika kutua katikati ya Ziwa Manyara lililopo Mkoani Arusha ili kunusuru abiria wake sita (6) waliokuwamo katika ndege hiyo baada ya kupatwa na hitilafu kwa kuzima ghafla kwa Injini moja wakati ikiwa hewani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Kamanda Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hilo majira ya saa 2.35 asubuhi maeneo ya Lambi, kusini mwa wilaya ya Babati.
Kamanda Sabas amesema rubani wa ndege aliyetajwa kwa jina moja la Kondo, ambaye hakudhurika katika ajali hiyo, alitaka kutua ghafla katika viwanja vya Arusha na Manyara baada ya kutokea hitilafu hiyo, lakini alishindwa baada ya kuona mtikisiko ukizidi na kuamua kuielekeza ndege hiyo katikati ya Ziwa hilo, ambapo alifanikiwa kutua salama.
Baadhi ya Boti na mitumbwi iliyokuwa karibu ilisogea na kutoa msaada wa kubeba abiria hao na kuwasogeza nchi kavu na baadaye ilifika Helikopta ambayo iliweza kutoa msaada zaidi.
Rubani tukupe hongera kwa jitahada kuokoa maisha ya wananchi na wahuisika wa vyombo kama hivyo kuweni makini kwa kufanya service ya uhakika kuepuka ajali zinazoweza kuepukika hongera rubani kondo
ReplyDeleteKondo namfahamu ni rubani mzuri sana. Niliwahi kusafiri kwa ndege yake mwaka 1989 tukiwa na mzee Aboud Jumbe mkewe na bodyguard wake akiitwa Abubakar Mbange. Kama ni Kondo huyu huyu basi ni rubani wa kutegemewa mzee huyu.
ReplyDeletePoleni kwa yaliyowapata abiria na hongera mzee Kondo kwa kuponya maisha na kuonyesha ukongwe wako angani
Hongera sana Rubani.
ReplyDeleteKondo umeonyesha umahiri na ujasiri uliotukuka ktk kuhimili tatizo lililojitokeza na kuweza kuokoa maisha ya abiria wako! Unastahili pongezi na sifa big up captain Kondo
ReplyDeleteCapt Kondo unastahili pongezi
ReplyDeleteMatendo yake Mungu ni ya ajabu sana. Tumpe sifa daima kwa kunusuru maisha ya ndugu zetu hawa. Hongera pia kwa Bw. Kondo kwa jitihada za pekee za kuokoa maisha ya hao abiria
ReplyDeleteMungu ameonekana pia, ni jambo la kushukuru, poleni kwa ajali ila pia hongeren mmepona. God is great. proscovia
ReplyDeleteGod is goodoo
ReplyDeleteYeah,God is good all the time..
ReplyDelete