Moto mkubwa unaripotiwa kuzuka asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyetta (JKIA) jijini Nairobi.
Chanzo cha moto huo bado hakijatambulika na juhudi za kuuzima zinaendelea, ambapo vikosi mbalimbali vya zimamoto vipo uwanjani hapo kuthibiti janga hilo.
Uwanja huo hivi sasa umefungwa na hakuna ndege kutua ama kuruka isipokuwa kwa dharura tu.
Moto huo unasemekana ulianza majira ya saa 11 za alfajiri sehemu za idara ya uhamiaji na kusambaa katika eneo la abiria wa kimataifa.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anaripotiwa kuelekea uwanjani hapo hivi sasa kukagua janga hilo, na habari zinasema hakuna mtu aliyedhurika kwa moto huo ingawa hasara iliyopatikana inasemekana ni kubwa na kwamba abiria wengi wamekwama uwanjani hapo. Barabara kuu ya kuelekea JKIA imefungwa.

Na habari zinasema kwamba baada ya saa tatu za ku pambana na janga hilo, hatimaye moto huo umeweza kudhibitiwa na hakuna mtu aliyeripotiwa kudhurika. Abiria waliokuwa wanasafiri wamepelekwa mahotelini na ndege zilizokuwa zitue JKIA zimeelekezwa kutua uwanja wa kimataifa wa Moi, Mombasa.
Moto Mkubwa ukionekana kutokea njia Kuu ya Kuingia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi,nchini Kenya
Shughuli Zote zimesimama Uwanjani hapo kupisha vyombo ya uokoaji kufanya kazi yake.
Wadau mbali mbali wakishuhudia Moto huo.

CHINI NI TAARIFA KUTOKA SHIRIKA LA NDEGE LA KENYA
We would like to inform all our customers and stakeholders that due to the fire at the Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) all our flights are currently cancelled until further notice.
All our staff and customers are safe and there is no damage to the aircrafts. The following flights landed safely in Nairobi: KQ765, KQ466, KQ221, KQ101, KQ625, KQ887, KQ732, and KQ417. In addition to this, five flights KQ117, KQ331, KQ311, KQ863, and KQ203 have been diverted to Mombasa. All our transit passengers are being facilitated to hotels in Nairobi and Mombasa.
One member of staff and a passenger had slight smoke inhalation and are safe in hospital for further investigation.
We will keep you updated as things unfold. For more information please call our contact centre on +254711024747/ +254734104747/ +254 20 3274747.
Dr Titus Naikuni
Group Managing Director and CEO
Kenya Airways
August 7, 2013

Ndugu zangu wakenya poleni kwa janga la moto,ninaimani hakuna aliedhurika. Ila nimevutiwa na jinsi taarifa za ndege zenu zilitolewa kwa haraka na pia nimevutiwa kuona wenzetu mna ndege nyingi kiasi hicho. wenzenu huku sijui tumelaaniwa na nani miaka yote hii ya uhuru tuna ka ndege kamoja na sijui kama kanafanya kazi.
ReplyDeleteMungu bariki uzalendo
Hata vyombo vya habari zikiwemo local radios za nje ya Africa zilitoa taarifa hivyo ya moto kwani ndege nyingi za nje ya Africa zimekwama kwenda Nairobi.
ReplyDelete