Mchezaji wa Mchezo wa Vishale kutoka Polisi Tanzania Julius Mwiru akicheza wataki wa mechi kati ya Tanzania na Angola wakati Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO nchini Namibia.Tanzania iliifunga Angola 34 kwa 2.
Mlinda mlango wa Polisi Tanzania Madopi Mwingira akiokoa mpira katika lango lake wakati wa mechi kati yake na Lesotho katika Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia.Tanzania iliifunga Lesotho 1 kwa 0
Washabiki wa Polisi Tanzania wakishangilia kwa kumbeba mwanariadha wa Tanzania Wilblado Peter baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za KM 21 katika Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia.
Wachezaji wa mpira wa pete kati ya Tanzania na Namibia wakipambana katika uwanja wa chuo cha Polisi nchini Namibia katika Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO nchini Namibia.Timu hizo zilitoka sare ya 29 kwa 29.
Picha na habari na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi
Wanamichezo wa Polisi Tanzania wanaoshiriki michezo ya nane ya Umoja wa wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia wameendelea kufanya vyema katika michezo ya mpira wa miguu,riadha, kurusha vishale na mpira wa pete kwa wanawake.
Katika mpira wa miguu, timu ya Polisi Tanzania imefanikiwa kuzifunga timu za Polisi za Lesotho 1kwa 0 na Angola 2 kwa 0 na hivyo kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.
Katika mechi na Polisi Lesotho timu ya Tanzania ilifanikiwa kuifunga Lesotho bao moja bila majibu huku bao hilo likipatikana kupitia kwa Winga machachari Nicholaus Kibipe katika kipindi cha kwanza.
Katika mechi na Angola mabao ya Tanzania yalifungwa na Ahmed Bello baada ya kutumia vyema mpira uliopigwa na Mokili Lwambo huku bao la pili likifungwa tena na Ahmed Bello kwa kisigino baada ya walinzi wa Angola kushindwa kuutoa mpira katika eneo la hatari.
Katika riadha watanzania waliibuka tena washindi katika mbio za Km 21 baada ya mkimbiaji wake Wilblado Peter kuchukua nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa lisaa 1:07:45 na hivyo kufanikiwa kunyakua medali ya dhahabu huku nafasi ya pili ikienda kwa Polisi Zimbabwe na nafasi ya tatu kuchukuliwa na Osward Revelian wa Tanzania aliyepata medali ya shaba.
Mtanzania mwingine Silvester Simon alichukua nafasi ya tano huku wanawake wakichukua nafasi ya sita na saba kupitia kwa Neema Emanuel nafasi ya sita na Fabiola Willium nafasi ya saba.
Kwa upande wa Mpira wa pete, timu ya Tanzania iliifunga Botswana mabao 46 kwa 17,na kutoka sare na wenyeji Namibia kwa mabao 29 huku ikipata kichapo cha mabao 45 kwa 17 kutoka kwa timu hatari na mabingwa watetezi Zambia.
Aidha katika mchezo wa vishale (dats) Tanzania ilizifunga timu za Polisi Kongo,Angola na wenyeji Namibia hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kuingia hatua ya fainali ya mchezo huo.


Polisi Tanzania DUME!
ReplyDeletePolisi Tanzania JEMBE!
''Wazee'' Bongo BUNDUKI!
Wamwela Bongo nomaaaa!
Manjagu wa kwa Jakaya wanatisha!
Polisi Tanzania si mchezo, kila siku mkiambia mnakataa oooh Polisi wa Tanzania wako vizuri ktk Kareti za Sherehe za Mahafali lakini wakiingia Mtaani si kitu kabisa, kwakwambieni nani?
Mnaona mambo yanayojiri Namibia huko?
Nchi zingine hazina Mafunzo ya Polisi kama sisi?
Ni kuwa wameiva kimafunzo ndio aana wanatesa Kimichezo.
Kufukuzana na Waporaji Keko, Kariakoo-Gerezani, Kariakoo-Jangwani, Kariakoo-Msimbazi na Kigogo Mbuyuni na Manzese mchezo?
POLISI TANZANIA NGUNGURI BANA KAMA ALIVYOWAACHA IGP MAHITA!
Polisi Tanzania huko Michezoni Namibia.
ReplyDeleteMsije mkapandisha Midadi ya kushinda hadi mkawafunga Pingu na kuwaandikia RB na Maelezo wapinzani wenu Polisi wa nchi zingine Michezoni?
Hiyo ni Michezo tu kumbukeni!
Si mchezo Polisi Tanzania inatesa hadi nje ya Mipaka!
ReplyDeleteIsipokuwa msije MKAWA ARESITI KATIKA MICHEZO HUKO NAMIBIA AMA MKAWAANDIKIA RB NA MAEREZO hiro ritakuwa ni kosa ra kiraiya na nje ya nchi na sio kosa ra jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mkizingatia mupo Namibia ni nje ya jamuhuri yetu...ni michezo tuu na kujiwekaga kamiri kamiri AU SIYO MWENZANGU SAJENTI MARWA?
Vibaka na Wezi Tanzania mmesikia Maafande wanavyotesa huko nje ya nchi?
ReplyDeleteKazi kwenu jiandaeni mtafute shughuli zinazo eleweka na kuchana na shughuli zisizo rasmi.
Wakirudi watakuwa kamili baada ya Mashindano ya Michezo mtashitukia wazima wazima mna mezwa na Mamba!
Hahahaha!
ReplyDeleteMdau wa Kwanza, nakumbuka ktk Jamvi humu Ankali aliturushia Polisi wakiwa ktk Mahafali waki piga Kareti na kuvunja matofali!
Wadau wakasema humu ya kuwa wakifika Mitaani baada ya Mafunzo wakianza kupokea Rushwa Ukakamavu wao wa kuvunja Matofali unayeyuka ghafla na mikono yao inageuka kuwa laiiini kama ya watoto wachanga!!!
Hongereni sana Polisi TZ, wapigisheni kwata kama za CCP hao! Tanzania oyeeeeeeeeeee!!!!!!!
ReplyDelete