Na Eleuteri Mangi – MAELEZO
Serikali imeanzisha mkakati wa kutokomeza wimbi la tatizo la dawa za kulevya nchini kwa kudhibiti viwanja vya ndege na sehemu mbalimbali za mipakani zinazotuhumiwa kupitisha dawa za kulevya.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo.
“Kwa yeyote aliyekuwa anafikiria kufanya biashara ya dawa za kulevya ajue muda wake umekwisha” alisema Mwambene.
Mwambene alisema kuwa tatizo hili litakuwa historia kwani ulinzi umeimarishwa, hivyo ametoa rai kwa mtu yeyote mwenye nia ya kufanya biashara hiyo aache mara moja.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa Serikali imeweka jitihada kubwa ya kutoa elimu kwa watumiaji na waathirika wa dawa za kuelevya ili waweze kubadili tabia zao za kutumia dawa hizo na kuwa watu wema katika jamii.
Aidha Mkurugenzi Mwambene amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter” kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.
“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete”, ameongeza Mwambene.
Assah Mwambene amefafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha Umma na si kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
kwa hiyo miaka yote hii kulikuwa hakuna mikakati ya kuzuia biashara za madawa ya kulevya kwenye mipaka yetu na viwanja vya ndege?
ReplyDeleteTanzania ndio yale yale jambo haliangaliwi hadi limfike celebrity au mtoto wa kigogo.
KWA MAANA HIYO TUSEME SASA RUSHWA PIA BASI.
ReplyDeleteHII NDIO TANZANIA!
NCHI YA MSINGI WA MANENO BILA VITENDO.
AIBU!!!!
Wanacheza hawa!
ReplyDeleteHaya madawa hayafai hata kidogo,serikali pambaneni nayo you have a wind behind you.Halafu nyie serikali imtafute huyu mtu (Mzungu?)aliyeandika hii habari kwenye miyandao ya kimagharibi awapeleke alikoona haya aliyoyaandika.Habari inafanana na ile Darwin Nightmare.Habari inaleta aibu kwa nchi yetu nzuri
ReplyDeletehttp://www.pbs.org/newshour/multimedia/harmreduction/
David V
Airport mmepiga vita dawa za kulevya, wizi wa mabegi umeanza rasmi. Juzi binti yangu amesafiri na Turkish Airline amekuta begi limechanwa na viatu (high hills) vimechukuliwa. Mambo haya sijui kama waturuki wana njaa za kuchana mabegi, it is only possible in TZ. Jinsi lilivyochanwa ni kama mtu alikuwa na haraka fulani hivi. Kwa hivyo ule mtandao wa hayo madawa ni mpana zaidi na inaelekea upo bado pale JNIA hivyo wana revenge kwa namna nyingine sasa. Wale vigogo hasa bado hawajafichuliwa.
ReplyDeleteAmini usiamini lakini the bitter fact ni kwamba madawa yanaingizwa kwa kupitia diplomatic cargo. Dawa zinazoingia airport ni chache mno na hii si hapa tu bali na nchi nyingi nyingine zinazolengwa. Huwezi kuamini lakini ukweli ni kwamba dawa zinatoka SHAMBA na kusambazwa moja kwa moja sehemu tofauti duniani kama silaha baridi. Kikulacho kinguoni mwako. Huu ni moja ya mipango maalumu ya masafa-marefu yanayolenga kudhoofisha baadhi ya nchi.
ReplyDeleteJinsi ya kupambana ni kuweka mkazo katika kuelimisha mashuleni hasa watoto wadogo. Pia kutumia pesa kufanya kampeni za kuelimisha wakubwa lakini siamini kabisa kama kuzuia peke yake kutasaidia lo lote.
David V!unaongea nini?Mara nyingi unaongea vitu vya maana lakini leo pumba kabisa. Sasa wamkamate huyo Mzungu ili iweje? Yeye kaongea na kutuonyesha tatizo ili tupambane nalo. Sisi wengine akina Yahaya tusingeweza kuongea ukweli ya haya kwa kuofia watu kama wewe kutupa kibano. Tusiwe wanafiki. Na kama tunavyoona Madawa na Ukimwi vinatuumbua. Unasema nchi nzuri, ("nchi nzuri my ..."-Sugu.Watu) wanakufa kila siku kwa ajili ya unafiki wetu.
ReplyDelete