KATIBU WA JUMUIYA ZA KIISLAMU TANZANIA SHEKHE ISSA PONDA NI KWELI HAPO JANA ALIPIGWA
RISASI NA KWASASA YUPO HOSPITALI YA
RUFAA YA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI NA SI KWELI KAMA YUPO CHINI YA
ULINZI WA POLISI KAMA SMS MBALIMBALI
KUPITIA SIMU ZA VIGANJANI ZINAVYOSAMBAZWA.PIA JUMUIYA NA TAASISI YA KIISLAMU
TANZANIA LEO BAADA YA SWALA YA ALASIRI KATIKA MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI ILITARAJIWA KUTOA TAMKO KUHUSIANA NA TUKIO HILO.
KATIBU WA JUMUIYA ZA KIISLAMU TANZANIA SHEKHE ISSA PONDA
KATIBU WA JUMUIYA ZA KIISLAMU TANZANIA SHEKHE ISSA PONDA AKIUGUZWA MUHIMBILI
SEHEMU ALIYOJERUHIWA KATIBU WA JUMUIYA ZA KIISLAMU TANZANIA SHEKHE ISSA PONDA
Watanzania jamani tusifuate mikumbo ambayo haina faida kwenye nchi yetu,naiomba serikali imchunguze huyu PONDA na kama ci raia wa Tanzania basi apewe masaa 24 ili atoke kwenye hii nchi,nakama atakua Mtanzania bc serikali imzibiti vilivyo huyu PONDA la sivyo mtu huyu atasababisha mauwaji ya wanachi wasio na hatia,why mtu mmoja tu atuponze sisi sote,na kama alikua katika KIFUNGO cha NNJE kwann afanye haya yote? Hii nikuonyesha ameidharau MAHAKAMA,POLISI,USARAMA WA TAIFA na SERIKALI kiujumla,jamani hivi serikali wapi inatupeleka? Nakuombeni wadau wenzangu mnisaidie kwahilo,,naitwa mdudu KAKAKUONA mm nailinda nchi yangu na kuipenda pia je vipi? Wenzangu nyie,asanteni nawapendeni wote watz,
ReplyDeleteSerikali isipoziba ufa itajenga ukuta.
ReplyDeleteMdogo wangu MDUDU KAKAKUONA usitie shaka SHEIKH PONDA yupo ALRIGHT KABISA na anayoyafanya yanamaslahi kwa NCHI thats why afaanya atakavyoo!We endelea tu na shughuli zako KAKAKUONA achana na mambo haya. Ponda yupo poa yaani ni bonge la CELEBRITY anapotupeleka ni pazuri sana kwa mustakali na maslahi ya taifa hilo. TUMEEANZA KUFUKUZA WANYARWANDA HILI MIMI NDO NAONA LA MUHIMU SANA MAANA WALA HAWAKUWA NA FUJO TUMEAMUA TU KUWATIMUA MAANA WAMEZUBAA. SASA TUNAHITAJI KINA PONDA WENGI TU ILI TUJIFUNZE
ReplyDeleteWewe kakakuona unamlaumu aliyedhulumiwa! Unajuwa amefanya au amesema nini huyo Sheikh Ponda kuhusu hicho kinachodaiwa kuwa "kuhatarisha usalama wa nchi.
ReplyDeleteHivi izi habari zinazosema kwamba shehe Issa Ponda siyo mtanzaniya zinatoka wapi? Na kwa nini isemekane asaivi? Watanzaniya acheni kusema vitu vyenye hamna uhakika navyo. Mimi naona cha msingi ni kuiombea nchi yetu amani na upendo maswala ya ubaguzi non.
ReplyDeletewanyarwanda wamejaa katika position kubwa kubwa serikalini, makampuni,na mabenki na wanajisifia na wanao umoja wao. nyie kalagabaho.
ReplyDeleteHISIA HISIA HISIA ! Bado watu wantakiwa kujua ukweli kuliko kusema yasiyokuwepo. Labda wengine hawana kumbukumbu. Huyu bwana alishaambiwa si raia tangu 1997 ! Lakini mara kadhaa sheria na taratibu za nchi zimethibitisha vinginevyo. Kama kuna wa kumlaumu ni sheria zetu ambazo zimeshindwa kumtia hatiani na kama sheria hamzitii hatiani basi tusihukumu kwa hisia kwani hiyo ndo hatari kubwa kuliko Ponda. Wanaweza kumuua Ponda kwa hisia. Kuna watu nyuma yake sidhani kama watakubali. Ni muhimu sheria itendeke na idhihike inatendeka. Kumhukumu mtu kwa tuhuma si sawa.
ReplyDeleteHalafu polisi wametaka kumkamata Ponda Morogoro au.....!? Maana alipotoka Zanzibar alikuwa Dar kwa nini hawakumkamata hapa na alioneka hadharani na kutangazwa kudhuria maeneo ya sherehe wakati huu wa Idd? Kuna nini Morogoro?
ReplyDeletewizi mtupu..Nimefanya kazi ya ya kuchunguza matukio yanayosababishwa na silaha za moto jeshini kwa miaka 9 sasa.Hili sio jeraha lililosababishwa na risasi.Ni porojo tu hapa.Huyu Ponda aueleze umma aliumia vipi hapo..Muonekano wa jeraha pamoja na sifa nyinginezo hapo zinaonyesha kilichotumika ni kitu ambacho pia licha ya kuwa na ncha kali lakini pia makali ya kukata na makali ya kukata yanajieleza vizuri na wazi zaidi hapo kwenye jeraha lake kuliko ncha..Maelezo yanahitajika zaidi na watu wa aina hii sio watu wa kuchekea hata kidogo.Kwanza yupo kwenye kifungo cha nje na bado anatumkia adhabu
ReplyDeletemie namuomba mheshimiwa rais aendelee kuwasaka hawa wanyarwanda popote walipo mpaka kieleweke
ReplyDeleteSheikh Ponda ameshauona udhaifu wa serilaki yetu na anautumia vilivyo.
ReplyDeleteEndelea Ponda kuiponda Tz. Wamekulea hivyo waonyeshe matunda yake.
jamani ushabiki hauleti tija .kiukweli ponda alikosea.sipendi na wala sijafurahia kwa tendo la kupigwa risasi na wala silungi mkono.abadan.{tukumbuke kauli hii aliisema nani?na kwa sababu gani?}unapotaka kufanya jambo tazama mwisho wake. ikiwa kuna kheri fanya nakama kuna shari acha.kuna kitu kimejificha kwa shekhe ponda na wanaomzunguka haya si maslahi ya uislam.kinacho takiwa kwetum wa islam tuangalie wapi tumejikwaa na nini turekebishe na wala si huko mnapo takaka kutupeleka kwa kuvaa joho na koti la kupigania haki za waislam.rejea nyuma katika kumbu kumbu kilicho tokea mwembe chai.nini kilianza na kuja kutokea kilicho tokea ..tusitazame tulipo angukia .tuangalie wapi tumejikwaa
ReplyDeleteshekhe ponda hayupo right kama msemavyo.mkumbuke alisha kosea katika jambo la msingi.alichotakiwa ni kurekebisha kosa alilo lifanya katika kesi yake ya mwanzo.na si vyenginevyo.nilisema kuna jambo lime jificha kwa shekhe ponda na baadhi yao.na ukitaka kujua hilo angalia alicho kitamka zanzibar kisha tazameni sosi yazanzibar ni nini?kuwa muislam haimaanishi ufanye kosa la kuvunja sheria ya nchi ama kwa uchochezi ama kwa vyovyote vile.kwa kutaraji uislam ilhali huoiganii uislam ila ni maslahi binfsi.narudia tena mazameni almarhum omar bashir mtazameni shekhe mbukuzi na wengine kama hao.walichokuwa wa kikisema kwa maemeo ya uislam kumbe kulikuwa na yasiri na allah akawabainisha .ponda hayupo sahihi.allah atampa shufaa nanguvu kisha atamjulisha yeye shekhe ponda na wenziwe ni wapi walipo teleza
ReplyDelete