Waziri Membe akiwasilisha mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba hoja ya kupendekeza uraia wa nchi mbili kuingizwa kwenye rasimu ya Katiba.Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Mh. Joseph Warioba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Mh. Jaji Augustine Ramadhan.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuujulisha Umma kuwa jana tarehe 26 Agosti, 2013, Mheshimiwa Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alikutana na Uongozi wa Tume ya Marekebisho ya Katiba.  Lengo la kukutana na Tume ilikuwa ni kuwasilisha pendekezo la haki ya Uraia wa nchi mbili kutamkwa na kutambuliwa kwenye Katiba mpya.

Mheshimiwa Waziri alikutana na Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Joseph Sinde Warioba, Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Augustino Ramadhani, Makamu Mwenyekiti wa  Tume pamoja na Katibu wa Tume na Naibu Katibu wa Tume.

Akiwasilisha hoja yake mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba, Mheshimiwa Waziri alisema yafuatayo:-
1.      Suala la Uraia wa Nchi mbili haliko kwenye rasimu ya sasa iliyotolewa.  Lengo la kufika Tume ni ni kuomba suala hilo liingizwe kwenye rasimu.

2.      Amependekeza Katiba itamke kwamba, Raia wa Tanzania aliyeko nje hatafutiwa uraia wake na mtu yeyote, chombo chochote sheria au Katiba, eti tu kwa sababu raia huyo amechukua uraia nje ya nchi.

3.      Katiba ikitamka hivyo, itungwe Sheria itakayofafanua haki, wajibu na masharti ya Mtanzania mwenye uraia wa nchi mbili.

4.      Katika kujenga hoja hizo tatu, Tume ilielezwa faida zitakazopatikana kwa kuitambua na kuishirikisha jamii ya Watanzania waliopo ughaibuni (Diaspora).  Tume pia iliondolewa wasiwasi juu ya madai kuwa uraia wa nchi mbili unahatarisha usalama wa taifa au utawafanya baadhi ya watu kupiga kura wakiwa nje. Tume iliambiwa kuwa Sheria za Uchaguzi hutawala upigaji kura kwa raia walio ndani  na nje na hauwi  holela.  Kuhusu suala la usalama, Waziri alisisitiza kama ni mashaka, basi mashaka hayo yawe kwa wageni wanaoomba uraia  nchini kuliko watanzania walioko nje.

Katika kumalizia, Mheshimiwa Waziri alisisitiza, “bado naamini watanzania walioko nje sio wasaliti, They are just  smart citizens”.

IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Big up! Mhe JKM na Mhe Membe!

    ReplyDelete
  2. I salute you Hon. Membe. We are smart citizens. There you are. To be able to run away from corruption, power outages, breakneck traffic jams, nuisance taxes and levies, muggings, road potholes, water shortages, dilapidated public transport, cold-blooded killings of business people, bodaboda drive-by shootings, bag-snatchers, pickpockets, etc. is not easy. Not many people can do that. Those who can do it must be smart.

    ReplyDelete
  3. Well said Minister Membe!

    Diaspora is a 21st century reality .... tukubali, tusikubali.

    Dunia kuwa kijiji ni ukweli usoyakinika. Hadidu za rejea ziliitaka tume kuangalia maslahi ya 'watanzania wote' ikiwemo wale wa Diaspora. Tume imetusahau kama tupo!

    ReplyDelete
  4. Great step kwa kweli. We need that, Naona Canada, Uingereza, Uyahudi na manchi mengine kibao yanaruhusu uraia wa nchi mbili. Lazma tuhamasishe uhamishaji wa ngawira toka nje kuingia TZ. ndivyo hata wakoloni walifanya na kukomba raslimali zetu kibao.

    ReplyDelete
  5. Asalam alaykum,
    Wadau wote tulioko njee inafaa kumpongeza sana waziri mheshimiwa Membe kwa kutufikishia swala ambalo tuna liomba kwamuda mrefu.
    Nawakati watu wa maoni wa katiba watakapo kuja ktk Nji tunazo ishi tuhudhurie kwawingi na tutoe maoni yetu.
    Nandugu zetu mulioko Taznzania tuungeni katka hili nahii nifaida kwetu wote.

    ReplyDelete
  6. Huu ni mtihani mkubwa kwa mwenyekiti wa tume kwakua alishatamka kwamba kisichokuwepo ktk rasimu hakitakuwepo ktk katiba,kuna suala la kadhi mkuu ambalo nalo linaombwa kuingizwa ndani ya katiba japo halipo ktk rasimu.Haya ngoja tusubiri busara.

    ReplyDelete
  7. Well said mhe. Membe!!!! Shukran maana naona wapinzani wa huko ulaya wanataka kuchukulia kama ni wazo la kisiasa kutafuta ushabiki,hili ni suala la utanzania,sio itikadi,nafarijika kama viongozi wetu wataliona hilo na kulifanyia kazi,shukran

    ReplyDelete
  8. Mh. Membe napingana nawa kwa kiwango kikubwa juu ya hoja ya usalama, kwa sasa ni mapema kuwa na uraia wanchi mbilia hapa kwetu Tanzania.... sababu moja ni hiyo ya usalama, kwa nchi za nje, ili wakupe uraia, ni lazima uukane wa kwanza, pale wanapokuruhusu kuwa na urai wa nchiu mbili, ni lazima maslahi ya kwanza yawe kwao sio nchi uliyozaliwa....tuende mbali huyo mtanzania mwenye urai wa nchi mbili, anakaweza kupenya na kuwa raisi wa nchi, huoni tutakuwa tumefika kwa waliyowakuka USSR 1990? unapozungumzia usalama usiwe na short term view.....ichukulia kwa muda mrefu... na ujiulize kwanini sasa hata hao USA wanakusapport kwa hili, jua wameona mbali na kuna jambo wanalitafuta Tanzania, ....statistic, zinaponesha katika miaka 100 ijayo tanzani ndio itakuwa na watu wengi zaidi Africa, kwanini? ni maliasili tulizonazo

    ReplyDelete
  9. Tusikimbilie kitu ambacho hatuna uhakika nacho,uraia wa nchi mbili utamsaidiaje mwananchi wa kawaida?Kama ni kuwekeza ukiwa na uraia wa nchi mbili sio sababu kwani tuna wazanzibar wengi wanaoishi kwa misaada(welfare)kam USA,UINGEREZA nk je huyu atawekeza nini?Tuangalie usalama na uzalendo kama baba wa Taifa alivyofanya

    ReplyDelete
  10. Wadau mliopinga uraia wa nchi mbili na kutaka kujua faida zake ni hizi hapa........Kuhusu usalama wa taifa sio kila mtanzania anataka urais,au uongozi wa siasa,bali haki yangu ya kuzaliwa Tanzania isipotee kisa nimepewa uraia wa nchi nyingine,na hiyo itasaidia vipi nchi yangu,Kwa mfano mimi naishi Sweden,Nina watoto wa Tatu,wamesoma elimu yao mpaka wamekuwa wataalam,mmoja daktari bingwa wa watoto,mwingine mtaalam wa kilimo na mwingine mfanya biashara mkubwa...siku moja wanataka kurudi Tanzania kufanya kazi na kuwekeza hawa kwa nini uwa hesabu ni wageni wakati baba yao ni Mtazania kwa kuzaliwa na walipata elimu yao nje na wanataka kutumikia nchi ya babu zao unashindwaje kuwatambua na kupata wataalam wa ziada?Katiba iseme wazi kuwa ukitaka kuwa Rais lazima uwe mzaliwa wa Tanzania na usiwe umechangia utaifa mwingine.Hapo tutasonga na kuendelea kama wenzetu Ghana,Namibia,Nigeria,Morroco na nchi nyingine nyingi tu na hapo ndio maendeleo ya kweli tutayaona.Naomba kuwakilisha.

    ReplyDelete
  11. Mheshimiwa Waziri Membe,

    Hongera sana kwa kulifikiria hilo na kulifanyia kazi. Watanzania tulio wengi hususan kwenye Diaspora ikiwa pamoja na kizazi chetu tunapoteza haki zetu za msingi tukiwa huku ughaibuni.

    Sheria iliyopo sasa inatubana! Uraia wa nchi mbili kwa watanzania tuliopo nje utatufungulia fursa zaidi za kisheria , kiuchumi, kijamii, kielimu na kimaendeleo na pia kuongeza fursa kwa vizazi vya kitanzania vinavyopatikana huku.

    Pendekezo hilo la Baraza la Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa litatuongezea watanzania tuliopo ughaibuni uhalali wa kisheria na wigo mkubwa zaidi wa kutumia fursa ambao kwa mfumo wa sasa na sheria zilizopo zinatubana.

    Mapendekezo ya Wizara yako yameangalia haki za kimsingi na maslahi ya watanzania wote bila kujali kama tupo ndani au nje ya nchi.

    Natoa pongezi sana kwa Baraza la Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kwako binafsi Mheshimiwa Membe na Rais Dkt. Jakaya Kikwete kwa kuliona hilo na kulisimamia. Hongereni sana kwa kazi na hatua nzuri.

    Mwisho natoa pongezi kwa Tume ya Mheshimiwa Jaji Warioba ina watu weledi, wasikivu na wanaoangalia maslahi ya Watanzania wote hilo nadhani watalipokea na kulifanyia kazi.

    ReplyDelete
  12. Nafurahi kuona maoni mbali mbali ya wadau tofauti. Kila mmoja amezungumza kwa kuzingatia maslahi ya Taifa letu. Kikubwa naomba tutofautishe uraia wa nchi mbili kwa Mtanzania mzaliwa(Maganga) VS mgeni kupata uraia wetu(Rajper).Maganga yeye hana shida kabisa, kwasababu uraia wake wa kuzaliwa atabaki nao, kazi kwake kuupata wa nchi nyingine kwa kufuata masharti ya hiyo nchi. Kama ni USA, basi afuate utaratibu wake lakini asipoteze uraia wa Tanzania. Nadhaani wachangia mada hapo juu hakuna anayemkataa Maganga kubaki na uraia wake. Sasa twende kwa Rajper, yeye anautaka uraia wetu, lazima afuate masharti yetu (magumu) kabla ya kuuchukua. Mfano kuna kitu kinaitwa birth rights ambavyo hata huku ughaibuni tunakumbana navyo. Kwa nchi yetu, kutokana na umaskini wetu, lazima tuwe makini kabisa. Birth rights aliyonayo Maganga asipewe Rajper. Maganga aruhusiwe kugombea nafasi za uongozi kisiasa, Rajper hapana. Mtoto wa Maganga apewe nafasi ya kuchagua once anapotimiza 20 years kati ya birth rights za TZ au za huko alikozaliwa. Bado anaruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili,lakini birth right achague. Rajper akipata watoto ndani ya ardhi ya Tanzania,na mmoja wa mzazi ni Mtanzania, basi huyo ni mwenzetu, apewe birth rights.
    Vitu kama investments, lazima brith right ifanye kazi, mwekezaji lazima atoe % kwa mzawa ili kulinda raslimali zetu. Kama ni madini,basi Rajper asiruhusiwe 100% kuinvest mwenyewe,lazima kuwe na mzalendo. Akijenga nyumba, basi anakodishiwa ardhi, lakini Maganga akijenga nyumba ni yake na ardhi ni yake.
    List ni ndefu,lakini lazima tutofautishe uraia wetu na Birth rights" ambazo laziwe zitajwe kwenye katiba.
    kazi nzuri Membe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...