Utangulizi:

Marais wa nchi za Rwanda, Uganda na Kenya, walikutana mwanzoni mwa mwezi uliopita, ambapo mojawapo ya maazimio ya mkutano wao, ilikuwa ni kufanya Mombasa kuwa kituo cha kukusanya ushuru, na hivyo Uganda na Rwanda waanze kusafirisha mizigo yao moja kwa moja kutoka Mombasa. (Angalia ambatisho)

Ufafanuzi:

Chama cha Umoja wa Wasafirishaji wa Malori nchini (TATOA), kinaamini hatua hiyo itadhoofisha uchumi wa nchi yetu kwa kiasi kikubwa sana.

Na kama serikali yetu ikipuuzia kujiondoa kwa wateja hawa wawili, Rwanda na Uganda, huenda nchi nyingine zaidi zikazidi kujiondoa kutumia bandari ya Dar es Salaam.

TATOA inaamini maamuzi kama haya ya nchi za wenzetu ya kurahisisha taratibu za ulipaji ushuru pamoja na kuboresha utaratibu wa bandari ni muhimu kwa bandari yetu pia.

Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) ilidhihirisha namna ambavyo bandari ya Dar es Salaam, ufanisi ukiboreshwa, inaweza ikawa mkombozi mkubwa wa uchumi wetu.

Faida za bandari hii kwa uchumi ni mtambuka, kwa hiyo TATOA haitapenda kuona mteja yoyote akijitoa kutumia bandari yetu, au kupungua kwa biashara kwa namna yoyote ile, na hivyo itapigania kwa kuishauri serikali katika kuboresha bandari yetu.

TATOA ni mmoja wa wadau muhimu kwenye sekta hii ya bandari, kwani biashara yake ni kusafirisha mizigo inayofika bandari ya Dar es Salaam kuwafikishia walengwa, hasa nchi zisizo na bandari (land locked countries) kama Congo, Zambia, Rwanda, Malawi,Uganda, Zimbabwe na Burundi.

Hivyo kuondoka au kupungua kwa namna yoyote ile kwa matumizi ya bandari yetu, ni hofu ya TATOA itaathiri uchumi kwa kiasi kikubwa.

Ieleweke kwamba, sekta ya usafirishaji wa malori ni muhimu kwa uchumi wetu. Sekta hii inatoa zaidi ya ajira milioni moja (1) za moja kwa moja, na nyingine zaidi ya milioni tatu (3) zisizo za moja kwa moja.

Sekta ya usafiirishaji wa malori pia, ni yapili kwenye uchangiaji wa pato la taifa (GDP).

Sekta hii pia, ni mojawapo ya sekta chache nchini ambazo zinagusa nyanja tofauti za kiuchumi kama, huduma za simu za kutuma pesa, matairi, spea pamoja na mafuta, ambazo zote zinafaidika na sekta hii.

Mabenki pia yamekuwa ni mojawapo ya taasisi zinazofaidika na sekta ya usafirishaji, ukiangalia kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, huduma inayoongoza kwenye mabenki ni Vehicle Asset Financing.

Zaidi ya hayo, TATOA pia inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye mfuko wa barabara, ambao ndio unatumika kuboresha barabara zetu nchini, kupitia matumizi ya mafuta, ambapo malori pekee yanatumia ziadi ya lita milioni mbili na laki tisa kwa siku kati ya lita milioni tatu na nusu.

Mwisho TATOA inaamini, uboreshaji wa reli ni muhimu kwa maendeleo ya sekta ya usafirishaji nchini, kwani miundo mbinu hii miwili, reli na barabara, inafanya kazi kwa pamoja.

Wakati reli inaweza kufikisha mzigo mpaka stesheni, malori yatahitajika kufikisha mzigo sokoni, au mahala pengine mteja atakapohitaji.

Mifano hai ni nchi ya Uingereza na Afrika Kusini, ambazo zina malori mengi pamoja na kuwa zina mfumo mzuri wa reli.

Lakini kwa nchi yetu, ambayo sekta ya reli bado inaboreshwa, tunaamini malori yataendelea kuwa na umuhimu mkubwa.

TATOA inaiomba serikali, kupitia wizara ya uchukuzi kufanyia kazi kero zilizopo katika bandari ya Dar es Salaam lakini pia kufanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wadau wa sekta ya usafirishaji.


========  ========  =======

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Rwanda ikikataa kutumia bandari itakuwa inajitia kitanzi yenyewe. HIzi hoja za kwamba tutaathirika hazina msingi wowote. Ni propganda tu za kuonenyesha kuwa Rwanda ni MUHIMU SANA kwa uchumi wetu jambo ambalo sivyo. Bandari ya Dar haipo kwa ajili ya Rwanda. Rwanda ni mengineyo tu. Bandari inaweza kufanya kazi na wenye magari kupata faida yao bila Rwanda. Acheni waende Mombasa. Pimeni mambo na hoja zetu kabla ya kutoa kwa umma.

    ReplyDelete
  2. Tamko la serikali please??.

    David V

    ReplyDelete
  3. Mteja ni mfalme(Tusisahau hilo)

    ReplyDelete
  4. Mnh! Kizungumkuti

    ReplyDelete
  5. Suala la kutumia bandari ipi siyo la kisiasa bali la kiuchumi zaidi. Kama gharama ya kutumia Mombasa ni kubwa msafirishaji mwenye akili hawezi kwenda huko.
    Pia maamuzi ya maraisi watatau ni ya kisiasa zaidi.
    Rwanda is the small economy in the world no matter how fast it grows in terms of %. Tanzania is the giant economy in terms of size and % growth. In sub-saharan Africa..after South Africa and Angola, Tanzania is following (in Size) so the effect of Rwanda's trade to Tanzania international trade is minor. Whether Rwanda like or not she will still depend on Tanzania beyond the port. food importation, education and transit to and from other countries will remain. In the free market, government cannot dictate the business to opt the port rather than the economic forces.
    While we need not to ignore the pull out of Rwanda and Uganda,...we need to strengthen further the efficiency of our port and infrastructure connecting the countries,

    ReplyDelete
  6. Mdau wa kwanza hapo juu sidhani kama una data au unasema kwa jaziba za tofauti tulizo nazo.Rwanda ni mdau mkubwa sana katika bandari yetu kwani miaka nenda rudi ametumia njia ya kati kwa kiwango kikubwa sana ndo maana hata Mh Raisi akasema Rwanda inaihitaji Tanzania kama Tanzania inavyoihitaji Rwanda.Serikali ishughulikie kero na wadau mjue ni wakati muafaka wa kufikira kiuchumi kama tunahitaji maendeleo badara ya kufikria kwa jazba na uamuzi usiokuwa na tija.Kila mmoja anajua mchango wa Rwanda kwa uchumi wetu.

    Mdau UK

    ReplyDelete
  7. mijitu mengine bwana inajisemea tu kweli shule ni muhimu,ati Rwanda wakigoma TZ haitoathirika basi hata elimu ndogo inakushinda?
    lISHAJIBIWA HILO...ILA

    Tanzania ielewe ina nafasi kubwa sana ya kuifanya bandari yetu ikatunufaisha kwa kuwa nchi nyingi kama somali Djibout hazina usalama sasa sisi ilikuwa ndio tumiliki east and central Africa kama tungeweza kutumia mbinu lakini sasa ndio hari jojooooo

    TRA wanajiona kama Mungu watu kama utafuata sheria basi weka miezi 3-5 ndio utasaidiwa lakini kama una bahshishi hapo utafanikiwa chap chap

    ReplyDelete
  8. Ni kweli suala la bandari si la kisiasa,na sidhani linapaswa kuhusishwa na tofauti za ki-siasa,Rwanada na Uganda zimechuku maamuzi staiki na si ya kukurupuka kwa kujali maendeleo ya nchi zao. Rwanda pamoja na mambo mengine inasifika kwa kukuza uchumi wake na pia kuwa na kiwango cha chini sana cha rushwa,ikilinganishwa na Tanzania. Matatizo ya bandari ni ya muda mrefu na wadau wamelalamika kwa miaka mingi-rushwa, upotevu wa mizigo,ucheleweshaji na viwango vikubwa vya ushuru. Wafanyakazi wa bandari wanaendasha makampuni ya clearence ambayo inapelekea mgongano wa ki-maslahi. Hatuwezi kukataa kwamba maamuzi ya kujitoa kwa Rwanda na Uganda ni pigo kwa Tanzania, na hatujui atakayefuata kujitoa ni nani. Rushwa,misamaha ya kodi,mikataba mibovu ya madini,madawa ya kulevya vitaipeleka nchi yetu nyuma ki-maendeleo miaka 60 iliyopita.Serikali inaona lakini kwa nini haichukui hatua, hakuna anyejua.

    ReplyDelete
  9. Tamko la Rwanda linakuja katika kipindi hiki ambacho uhusiano umepwaya kwa namna moja ama nyingine. Kwa mantiki hiyo wanaitumia fursa hii kama kitisho kwa Tanzania. Kwa anayeijua tabia ya vitisho ya Rwanda atauona ukweli huu. Na ujumbe kwa ni kwamba Tanzania haitishwi. Wakitaka waache. Wataathirika zaidi ya Tanzania na si vinginevyo. Na kama marais hao wameamua hivyo huo ni uamuzi wao. Sasa mnataka Rais Kikwete naye awaite kuwabembeleza watumie Dar? Hilo halipo. Waambie waache leo hii ila tambua kwamba watarudi tu. Watakwenda wapi?
    Suala la Tanzania kuboresha bandari zetu hilo halina ubishi na tayari serikali inafanya kazi hiyo ikiwemo ya kujenga bandari mpya Bagamoyo na kuzifanyia ukarabati Tanga na Mtwara.

    ReplyDelete
  10. Nafikiri muhimu ni kuboresha ufanisi wa bandari, barabara na reli uwe wa kiwango cha kimataifa. Wateja watakuja wenyewe huduma zetu zikivutia.

    ReplyDelete
  11. Nafikiri mizigo ya eastern DRC ni mingi zaidi kuliko Rwanda ikiwa itakua na amani...Rwanda ni very tiny country inayojikuza tu ...hatutatetereka kwa kinchi hiko kuhamia Mombasa...ndo maana tunataka DRC iwe shwari tufanye biashara tuachane na hawa banyamulenge waende Kenya!

    ReplyDelete
  12. LAKINI TAARIFA YA HAPO JUU ILIYOTANGULIA KABLA YA HABARI HII MBONA INASEMA BANDARI DAR MAMBO SHWARI TU NYIE MNALIALIA NINI HAPA?KAMA WAMEAMUA KUFICHA UKWELI WAKIDHANI HAITAJULIKANA BASI WATAUMBUKA TU SI MDA MREFU.

    ReplyDelete
  13. sasa unajua kuwa akiwa na matatizo ndio akili inatakiwa kufanya kazi kwa kutafuta nia mbadala wake,,sio kweli kwamba uchumi wetu utapwaya kama mnavyochangia walio wengi,, kwani nchi yetu si masikini mpaka kweli tuathirike na kujitoa hawa jamaa,,hakuna kitu waache wafanye mambo yaop cha msingi sisi tujirekebishe kama kulikuwa na matatizo ili nchi nyingine tofauti na hizo zitumie bandari yetu,,na tutafute njia za kukuza uchumi bila kumtegemea mtu mwingine nchi yetu ni kubwa sana inalisosi nyinyi sana sio lazima Rwanda na Uganda wawe patina wetu sio kweli..cha msingi akili tulizopewa na mungu ndio tuzitumie ukiwa hujapata matatizo huwezi kufikiria vyema,na maisha ndivyo yalivyo kesho yanakuwa hivi leo inakuwa hivi hivyo hapo hakuna mtu wa kumlaumu hakuna siasa wala nini tupige kazi nchi zitakazohitaji kushikiana nazo zitakuja baada ya kuona kazi tunazofanya ni njema na asiyetaka aache ,,nchi inajengwa na wananchi na sio wengine,,,sisi mkae mkielewa nchi jirani zetu ni maadui kataa kubali ukweli ndio huo,tuondoe uwoga wa kusema biala fulani hatuwezi sio kweli tunaweza kufanya kila kitu bila hawa jamaa kabisa,,mungu mbariki kila mtanzania na Tanzania,mawazo yawe bora zaidi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu ,,mwaaaaaaaaaaaaa tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...