Tume ya Mapendekezo ya katiba kwa watanzabia wanaoishi Marekani imeundwa ili kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa watanzania wore waishio nchini Marekani na Canada.
website http://www.katibatanzania.org
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
KWA KWELI NAOMBA MSISAHAHU KUINGIZA SWALA LA URAIA WA NCHI MBILI.Vinginevyo mapambano nje ya nchi kwa wale wenye uraia wa kigeni itakuwa sawa na kutwanga maji kwenye kinu.Hawa jamaa wanatakiwa waelezwe umuhimu wake na kama wanaogopa wahindi wanaweza kufanya reform katika kipengele hicho kwa kuwapa raia waliozaliwa Tanzania tu, au wakafanya marekebisho mengine etc, etc.
ReplyDeleteHatutaki habari ya uraia wa nchi mbili. Watanzania wenye uraia wa kigeni hawafiki hata 2% ya watanzania wote. Kuna mambo ya msingi zaidi ya kujadili kuliko hili la uraia wa nchi mbili.
ReplyDelete"hatutaki uraia wa nchi mbili", wewe na nani? Fungukaa
ReplyDeleteHata nchi zilizoendela zipo ambazo hazina Uraia wa nchi mbili.
ReplyDeleteMsilete Hoja ya kuwa kuwa na Uraia wa nchi mbili ndio msimamo wa nchi zote zilizo endelea Dunia nzima. \
Kila kitu kina faida na hasara zake.
Ndio kama suala la Uraia wa nchi mbili lina pande mbili za sarafu FAIDA na HASARA:
Nafafanua kwa ufupi:
1.FAIDA:
-(REVENUES) MAPATO YA KUHAMISHIKA YA KIFEDHA NA MITAJI''Foreign Remittances from Diaspora communities abroad'', Bonds, and Shares, Equities and Cross trading of securities. Mzunguko wa Biashara za Hisa utainufaisha nchi watakapo amua kuhamisha Mtaji na amana kuja Tanzania ama kutoa Tanzania na kuuza nje ya Tanzania kwa faida.
-TECHNOLOGY TRANSFER
Uhamishaji wa Teknohama kuingia nchini.
-PATENT AND INTELLECTUAL PROPERTY
Upataji wa haki miliki na Tija kwa kazi zilizo fanywa na Watanzania nje ya nchi kuinufaisha Tanzania.
2.HASARA:
-(TAX EVASSION and CRIME) UKWEPAJI KODI NA UHALIFU, Wanaokaa nje ya nchi huweza kufanya Uhalifu nchini kwao na huweza kukwepa Kodi kwa kutumia mwanya huu, inaweza kutokea huko waliko waka claim wanalipa Kodi huku Tanzania wakati hawalipi hivyo wasilipe Kodi kotekote( Hii inategema na Mfumo wa Kodi kwa kila nchi ya Dunia lakini hii ni General kwa nchi zote)
-ESPIONAGE AND NATIONAL SECURITY,(UHAINI) Kuna hatari kwa Usalama wa nchi endapo Mwana Diaspora ataihujumua ama kuihatarisha nchi Kiusalama kwa maslahi binafsi...ama endapo Mwana Diapsora naweza kutumiwa na wengine huku akiwa hajielewi kuiponza nchi yake ama kuihatarishia nchi kama yaliyo kuta EDWARD SNOWDEN na Marekani.
-SOVEREIGN PROTECTION:
Inaweza kutokea mtu mwenye Uraia wa nchi mbili akakingiwa kifua na nchi yake ya pili anapo tenda kosa nchi moja hivyo kukwamisha juhudi za nchi moja kumuwajibisha Kisheria.
-ECONOMIC SABOTAGE:
Mtu mwenye Uraia wa nchi mbili anaweza kuihujumu nchi moja kanufaisha nyingine kama anavyoweza kuhamisha Mitaji na Mapato.
-NATIONALISM: Mara nyingi mtu anapohama nchi hutoka akawa hana interest tena na kwao, na ndio maana nchi nyingi zenye kuwa na Uraia wa nchi zaidi ya moja hazitoi nafasi ya Unongozi wa Juu kama Uraisi kwa mwenye Uraia Pacha kwa kuwa wanaamini mwamko wao wa Uzalendo umepungua ama utakuwa ume lega lega na kwao ingawa hii sio kuwa ndio kila Mwana Diaspora hana Uzalendo na kwao, inawezekana akawa na Mapenzi nakwao pia ikawa kinyume chake...NADHANI MADIASPORA WA TANZANIA WANGALI WANAIPENDA NCHI YAO YA ASILI TANZANIA.