Mwenyekiti wa Yanga-Yusuph Manji
---

1. Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu (Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016
2. Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha kuwa mkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGA zisirushwe hewani na Azam Media.
Kwa kuwa wawazi, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA kupitia vyombo vya habari tarehe 29 Julai, 2013 ambapo iliweka bayana sababu zake na kueleza kuwa YANGA haina tatizo na vilabu vingine vya mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake za Vodacom Premier League katika Azam Television.
Sote tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya ziada” inatumika kupotosha msimamo wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha Klabu ya YANGA hadharani.
Juu ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu ambavyo vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu, havina uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati ya Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu zinazojionyesha wazi.
Inadhihirika wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama kuilazimisha YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.
Kwa kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu.
Kwa kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi waje tujadiliane na kuamua suala la Azam Television kurusha mechi za YANGA.
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB


Kutokana na utajiri wake Yusuf Manji ni kama mfalme ndani ya Yanga na lolote alitakalo ndio litakalokuwa!! Sasa kwa kuwa Manji hataki suala la mechi zake kuuoneshwa na Azam TV pamoja na kuwa ni suala la manufaa kwa wananchi wengi na pia faida kwa Yanga yenyewe, hilo jambo halitakuwa, hivyo huo mkutano unaofanywa hauna maana na faida yoyote zaidi ya baadhi ya wanachama kujikomba na kujipendekeza kwa huyo Yusuf Manji.
ReplyDeleteKwa ufupi as long as Yusuf Manji doesn't like Azam TV coverage for Yanga matches then none will be able to change Manji's stand even thousand members since Manji's influence to Yanga is more superior than the majority of members!!!!!!!!
Wacha kuchezea mwenye pesa bwana.
1st annony remember Yanga can make Azam TV's fee in just one match. It is unfair deal to give Yanga just 100m for telecasting all its matches.Let Azam deal with the rest. After all Azam has a team in the league its better this done by another independent media.
ReplyDeleteUyanga na Usimba ndio unaodumaza soka la Bongo,yaani ubabaishaji mtupu!!
ReplyDeleteKamwe TZ mpira hautaendelea kwa aina ya viongozi kama Manji. Ndio maana juzi CAF imetoa list ya vilabu bora Afrika Yanga haipo hata kwenye 370 bora. Ubishi tu umeja, walikataa kucheza na Simba CECAFA, mara wakagomea jezi, mara hatutaki kushiriki kombe la muungano. Hii sio timu, ikacheze ligi yake yenyewe, mmechukua ubingwa mara 60, huko CAF kwa wanaume wenzenu mmechukua mara ngapi? Acheni ushamba.
ReplyDelete