WAKALA wa Barabara Mkoa wa Mwanza(TANROAD) hatimaye imeanza utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete na serikali kwa kuanza mradi wa ujenzi wa barabara ya Lami ya Usagara hadi Kisesa yenye urefu wa kilomita 17.8 ili kupunguza msongamano wa magari makubwa na madogo kuingia Jijini Mwanza.
Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mwanza Mhandisi Leonarld Kadashi alisema serikali baada ya kupata fedha ilitangaza kazi na kupatikana Mkandarasi aliyeshinda ambaye ni Kampuni ya kizalendo ya Nyanza Road Works Ltd ya Jijini Mwanza ambapo kwa sasa Mkandarasi huyo yupo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa barabara hiyo ya Usagara-Kisesa ya kiwango cha lami.
“Kazi imeanza tangu mwezi Julai mwaka huu na inaendelea kwa kasi na tayari Mkandarasi aliyopo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa barabara hiyo anaendelea na kazi ya kusafisha barabara ambapo kilomita 5 tayari na ujenzi wa madaraja sanjari na ujenzi wa nyumba za kambi ya Mhandisi mushauri na msimamizi na wafanyakazi wake kisha kuendelea na ujenzi wa kuweka lami”alisema




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...