Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac J. Nantanga akizungumza na Waandishi wa
Habari jijini Dar es Salaam kuhusu
mafanikio yaliyofikiwa na Tanzania kuwarejesha kwao wakimbizi waliokuwa hapa
nchini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Uratibu wa Mawasiliano ya Serikali, Bi. Zamaradi Kawawa.
-----------------------------------
Serikali ya Tanzania imewarejesha kwao kwa hiari
wakimbizi wapatao 569,018 toka nchi
za Maziwa Makuu waliokuwa wamehifadhiwa hapa nchini kutokana na machafuko
katika nchi zao. Kati ya hao 502,358 walitoka nchini Burundi na 66,660, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo. Wakimbizi hawa wamerejeshwa kwao
kufuatia zoezi lililoanzishwa rasmi mwaka 2002 kwa wakimbizi toka Burundi na
mwaka 2005 kwa wakimbizi toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRS), baada ya
usalama katika nchi zao kuimarika.
Sambamba na mafanikio haya, pia kambi
12 kati ya 13 zilizokuwa zikitumika kuwahifadhi wakimbizi hawa zimefungwa, na
hadi sasa ni kambi moja tu ya wakimbizi ya Nyurugusu, wilayani Kasulu mkoani
Kigoma ndiyo iliyobakia ikiwahifadhi wakimbizi kutoka DRC (63,728), Burundi (4,153)
na nchi nyingine mchanganyiko za Kiafrika
(212).
Tanzania inajulikana kimataifa kama
nchi mojawapo ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kutoa hifadhi kwa wakimbizi
wanaokimbia nchi zao kutokana na machafuko ya kiaiasa ambapo mwaka 1995 idadi
yao ilifikia zaidi ya milioni moja.
Lengo la Serikali ni kuona kuwa suala
la kuhifadhi wakimbizi hapa nchini linafikia ukomo na juhudi zinaendelea kuona
kuwa hata Kambi ya Nyarugusu ambayo ndiyo kambi pekee iliyobakia inafungwa
baada ya wakimbizi walio katika kambi hiyo kurejeshwa kwao, pale hali ya
usalama nchini DRC itakapokuwa imeimarika.Kuondoka kwa wakimbizi hawa sasa
kunatoa nafasi kwa Serikali na wananchi kutumia kwa shughuli nyingine za
kimaendeleo maeneo makubwa yaliyokuwa yanatumika kuhifadhi wakimbizi, lakini
pia kunatoa nafasi nzuri ya kuweza kukabiliana na changamoto za kiusalama
katika maeneo hayo ambayo yapo katika mikoa ya mpakani mwa nchi.Serikali inapenda kuishukuru Jumuiya
ya Kimataifa kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR), kwa misaada ya hali na mali waliyotoa na wanayoendelea kutoa kusaidia
hifadhi ya wakimbizi hapa nchini. Pia Watanzani wote na hasa wale wa mikoa ya
Katavi, Kigoma na Kagera kwa ushirikiano waliotoa kwa wakimbizi waliokuwa
wamehifadhiwa katika maeneo yao, na nchi za Burundi, Congo kwa ushirikiano wao
uliowezesha kuwarejesha raia wao waliokuwa wamehifadhiwa hapa nchini.
Mashirika mengine ambayo pia
yalihusika na yanaendelea kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi ni pamoja na
Shirika la Chakula Duniani (WFP), Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto
(UNICEF), Kamati ya Kimataifa ya Uokozi (IRC), na Shirila la Msalaba Mwekundu
Tanzania (TRCS).
Imeandaliwa
na Felix Mwagara
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
nyinyi wabaguzi tu hamna lolote !!wapeni uraia waafrika wenzenu, kama nyinyi mnavyolilia uraia nchi za ulaya na sio kuwarudisha makwao
ReplyDeleteNdo tushawarudisha, we unasemaje sasa? Ushaambiwa kwa hiari hawakushikiwa mtutu wa bunduki, bora kwa maana tunawahifadhi miaka na miaka mwisho wa cku wanatugeuka.
DeleteWewe sasa nikosa mtu kumrudisha kwao na kama ni ubaguzi acha ufanyike,kwani IZRAEL SI NAO WANAWARUDISHA WAETHIOPIA NA SIO TIO NA NCHI ZINGINE,WEWE WATU WOTE HAO UNAWEZA KUWAPA URAIA,,WOTE? NCHI GANI DUNIANI IMEFANYA HIVYO AU NA WEWE NIMYARWANDA UNALETA CHUKI ZA BINAFSI.SEMA NI NCHI GANI IMETOA URAIA KWA IDADI KAMA HIYO ,RAIS WETU JUZI KASEMA KASHATOA URAIA KWA WAKIMBIZI WENGI TU SASA WEWE UNATAKA NINI?-UPOLE WETU NDIO UNAFANYA NYIE WENGINE MNAKOSA SHUKRANI KWA MUDA AMBAO WALISHAKAA NCHI ULITAKIWA KUSHUKURU KUWA WAMERUDI SALAMA NA WALIKUWA HAWABUGUDHIWI.SASA IMEKUWA SHUKRANI YA PUNDA.SISI TUMEFIKIA HAPO KAMA UNAWEZA WAPELEKE NCHINI KWENU
ReplyDeleteAcha warudi kwao,majitu yenyewe yanasaidiwa then yanarudi kumtukana rais wetu JK,hao hao wakimbizi wameongeza ujambazi mikoa ya Kagera na Kigoma.Hata waliobaki nao warudishwe kwao tu maana hawana shukrani hata kidogo kushinda punje ya haladari
ReplyDelete